Home Traders

Home Traders

Tembelea TK FM Redio 88.5 Tanga

Saturday, 30 August 2014

Kwanini mtu anaetokwa na damu puani halazwi chali?

Msomaji wa tanga kaunani kwa mara nyengine basi kama ilivyo desturi yetu wana tanga kwa kukumbushana mambo muhimu basi leo tunawakumbusha jinsi gaani mtu anayetokwa damu puani kua huruhusiwi kumlaza chali yaani kuangalia juu.Tanga Kunani ilipiga stori na Dokta Othman Mkumba kutoka St John Ambulance ambaye anatupa faida kubwa sana kuhusu hili kwasababu jamii iliyotuzunguka tulikuwa tukifahamu kua mtu akitokwa na damu puani ili damu ziweze kukata zisitoke basi eti tulikuwa tukisema mlaze chali eti nduio damu zinakata...haaaaaaa kumbe hii ni hatari kubwa sana tena sana na inaweza kukupelekea hata kifo,sasa hebu tuungane nae Dokata Mkumba akitufahamisha kwanini basi watu wanatokwa na damu puani.
Tanga Kunani:Dokta tungependa kufahamu ni kwanini basi watu wanatokwa na damu puani?
Dokta:Kutokwa na damu puani ni matatizo ya kawaida ambayo inawatokea watu na si kitu kigeni,hii ni  inatokana na vishipa vidogo vidogo vilivyopo ndani ya pua kupasuka na vikipasuka basi damu hua inatoka puani.

Tanga Kunani:Dokta kuna hili tatizo la mtu akitokwa na damu puani tuna mlaza chini je tupo sawa kufanya hivi?
Dokta:Hakika kuna madhara ya mtu akitokwa na damu puani ambapo tumezoea sana katika jamii yetu,kwani haitakiwi kumlaza  mtu chali kwasababu damu inayotoka katika vishipa vidogo vya damu inatakiwa itoke nje sasa unapomlaza chali ina maana unaizuia  damu hiyo inayotaka kutoka  nje isitoke  na iende ndani  ambapo kule ndani inapokwenda haitoingia katika vile vishipa vya damu inapotoka kwani itaikwenda sehemu nyengine ya mwili na ikifika kule  itaganda kwa sababu haina virutubisho na ikiganda itaoza na ikioza itasababisha kutokea kwa bakteria  ambapo utapata madhara au magonjwa  ili tusipate madhara basi tuiache damu itoke nje.
Tanga Kunani:Shukrani sana Dokta ila wakati mwengine ntakutafuta ili tuzungumzie kwa undani kuhusu mtu kutokwa na damu puani ama masikioni pamoja na visababishi vyake.
Kumsikiliza DoktaBofya Hapa

No comments:

Post a Comment