Home Traders

Home Traders

Tembelea TK FM Redio 88.5 Tanga

Saturday, 30 August 2014

Lijue soko la Tangamano kwa kulipua wakina dada!

Na Kassim Discover
Naaaaaaaaaaaam msomaji wa tanaga kunani leo kwa mara nyengine katika safu yetu hii nakuletea soko kubwa,bora na muhimu sana kwa wana Tanga na hata nadiriki kusema mkoa wote wa Tanga maana takaribani asilimia kadhaa wananchi toka nje ya Tanga pia hujitokeza kuja kutafuta mahitaji yao ambayo watoto wa mjini huuita kujipigilia Viwalo.
Haya bwana tuachane na hayo tuanze sasa safari yetu ya kukupeleka katika soko hili la Tangamano ambalo wakati linaaza hakuna alieamini kama lingeweza kufikia kiwango hiki kwa siku hizi maana soko hili linakuwa kila kukicha,ni soko lililowakomboa vijana na wana Tanga wengi kimaisha kwani Biashara inayofanyika hapa sia ya mchezo ni biashara babkubwa ambayo inadiriki mwana Tanga kusongesha maisha yake mbele huku akisomesha watoto na kulea familia yake bila kutetereka.
Wapo waliofunga maduka yao na sasa wakilitumia soko hili kwa uzuri kabisa,hakika soko hili la Tanga mano kwa sasa linafanya kazi siku za jumamosi,jumanne na Alhamisi wakati hapo awali soko hili lilikuwa likifanya shughuli zake mara mbili tu kwa wiki ambazo ni siku za jumamosi na jumanne,sasa hapa si ndo tunadiriki kusema kuwa soko la Tangamano limekua tena kwa kiasi kikubwa kweli.
Utafurahi sana mwana Tanga pale inapokaribia msimu wa sikukuu jinsi soko hili linavyotapika huku wataalamu wa biashra wakilifananisha na soko la KARUME pale jijini Daresasalaam.
Hivi ni nani anaebisha kuwa mwana Tanga akijipiga viwalo vyake jinsi anavyotokeleza na kupendeza na hata kuvutia kwa jamii? hilo halipingiki na ka ma halipingiki basi utakuta wanadada wa kila aina wakiwemo wanafunzi siku za jumamosi au jumanne jioni wakijilipua katika soko hili la Tangamano kwa kujichaguliwa viwalo vyao bwana...daha utawapenda pale wanapojipigilia?

hebu cheki akijimwaga baibui lake safi huku akijipigilia shungi lake si ndo utampenda mtoto wa Kitanga anavyopendeza.Haya tuachane na hao dada zetu hata wavulana nao pia wajipigilia bwana viwalo vyao tena vile vijinzi vyao wanavyovipenda siku hizi vya kujibana bana na juu akijipigilia  flana yake hata ya buku au buku mbili daaa nao pia si utawapenda,hakika soko hili la TANGAMANO ni mkombozi mkubwa sana kwa wakazi wa mkoa wa Tanga.
Asante sana Kapten  Mkuchika sambamba kabisa na ujio wa vidala dala wakati vilipoanza watu walidharau kweli lakini leo hii ni usafiri imara na unaoaminika mkoani Tanga.
Hahahahahahahahaha wacha nicheke bwana sijamaliza hebu wafanyabiashara nao wa soko hilo walivyo safi,ukarimu wa kukaribisha wateja,bashasha juuu dahhhhhh kweli bwana wana Tanga tumo.
Mi sina la ziada kwa leo hebu ngoja nielekee hapo TANGAMANO si wajua siku ya kujilipua leo jumamosi!
KARIBUNI SANA TANGA!!

1 comment: