No Cd,No Memory,No Flash hayo si maneno yangu ni maneno ya watangazaji wa kituo bora cha matangazo cha TK FM kilichopo hapa hapa Tanga AMBAPO SIKU YA JANA WALIFANYA BONGE MOJA LA SUPRAIZ kwa wasikilizaji wao baada ya kujaribu vipaza sauti tangu ilipokua hewani mwezi mmoja uliopita.
![]() |
Meneja wa TK FM Said Karsandas |
Ni kituo bora kilichokua na vifaa bora kiukweli hata ukibahatika kuingia utaamini maneno yangu kua ni kituo bora na watu kweli wamewekeza vya kutosha.
Sauti ya kwanza kusikika hewani ilikua ni ya DJ mwenye swaga za kutosha na anaekubalika vya kutosha awapo katika mashine si mwengine Dj Rogie Kisie ambae ndio alieanza kuwatambulisha wenzake huku Bosi mtoto Meneja wa kituo hicho Said Karsandas Pandram akifunguka vya kutosha kuhusu malengo ya TK FM.
![]() |
Mkali wa Mixing DJ Rogie Kissie |
Karsandas akizungumzia uwekezaji mkubwa uliofanyika katika kituo hicho amesema kua wana vifaa bora vilivyomo katika studio hiyo huku akisema pia wamekuja kufanya kazi,aidha pia aligusia kuhusu ufunguzi wa kituo hicho ambapo utafanyika kabla ya disemba 25 mwaka huu huku ukianzia maeneo mbali mbali ya mji wa Tanga na mwisho ni bonge la shoo litakalohusisha wasanii wakubwa wa nchi hii.
Katika siku hiyo ya jana studioni palikuwepo vichwa vya kutosha kama vile Meneja mwenyewe Said Karsandas,Dj Roggie Kisie,Leyla Toty Inginia wa jiji sonara wa maneno,binti mwenye sauti ya kushiba ya Radi Mboni Muya huku Dj Eddy Mix akiwa na hudhuru siku ya jana,hata hivyo baadhi ya wakali waliowahi kufanya poa katika baadhi ya vituo vya Redio wakitajwa kuwa katika timu ya maangamizi.
TK FM mapema kabisa siku ya jana ilianza harakati zake kwa kugawa stika za TK FM kwa vyombo vyote vya usafiri jijini Tanga bureeeeeeeeeee huku ikiwaahidi wasikilizaji wake Tshirt itakazo zitoa kwao ukikutwa tu unasikiliza TK habari ya mujini.
Kwa upande wa wasikilizaji wamesema kua TK FM imekuja kuleta mapinduzi makubwa mkoani Tanga na heshima ya Tanga imerudi iliyokuwa imepotea kwa miaka kadhaa.
Lichaya yote pia wasikilizaji walifurahishwa kuwasikia tena katika vipazasauti vyao wakali hao waliotamba na baadhi ya Redio hapa Tanga na baadhi ya Rediokwa kuzipa mafanikio ya hali ya juu.
TK FM ni Redio pekee inayosikika bila ya chenga na ndo maana ukaja msemo huu No Cd,No Memory,No Flash na pia niRedio pekee inayosikika takribani wilaya zote kwa sasa ukiondoa kituo cha kidini cha Ihsaan Fm.
Wakali hao walivitaja baadhi ya vipindi vitakavyokuwepo kama vile Afro Dances,Chambu Chambu,Nakshi za Pwani,Inter Spotrs na vinginevyo bora kabisa.
Mungu ibariki TK FM ifikie malengo yake!
No comments:
Post a Comment