Home Traders

Home Traders

Tembelea TK FM Redio 88.5 Tanga

Friday, 5 August 2016

Warembo wa Tanga kuwavaa wenzao miss kanda kesho

Warembo takribani watatu watakaowakilsha  mkoa wa Tanga katika fainali za miss kanda 2016  watawakabili wenzao zaidi ya kumi kutoka mikoa mbali mbali ya kaskazini kwajili ya kuwapata wawakilishi watakaoiwakilisha kanda ya kaskazini kitaifa.
Fanali hizo za kanda zitafanyika katika ukumbi wa TRIPLE A jijini Arusha na kutumbuizwa na msanii wa bendi ya fm academia NYOSHI AL SADAAT HUKU KIINGILIO KIKIWA NI SHILLINGI 10,000/= NA vip 30,000/=

Warembo toka Tanga wanaoiwakilisha Tanga ni mshindi Elgiva Mwasha,Asha Ally alieshika nafasi ya pili na Rukaiya Hassan aliyeshika nafasi ya tatu.

Hata hivyo blog hii imemtafuta Bi Mboni Muya ambaye  alikuwa ndio mratibu wa miss Tanga akiwa safarini kuelekea Arusha kushuhudia fainali hizo amesema kuwa  warembo hao kwa sasa wapo kambini na  wana Tanga wawaombee kwa ajili kuiletea heshima mkoa wa Tanga huku akisisitiza kuwa warembo hao watafanya vyema na kuipepereusha  Tanga.

Naye mwandaaji wa onyesho hilo Faustine Mwandago  alisema kuwa katika show hii atahakikisha washabiki wote wanaifurahia  show hiyo. 
Habari Hii imeandikwa kwa msaada wa KASSIM DISCOVER,MBONI MUYA pamoja na Michuzi  Blog.

No comments:

Post a Comment