TIMU ya taifa ya
vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’, kesho itashuka dimbani kumenyana na wenyeji Afrika
Kusini katika Uwanja wa Dobsonville ulioko Soweto, kwenye mchezo wa awali
kuwania nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, zitakazofanyika
Madagascar mwakani.
Kocha mkuu wa Serengeti boys Bakari Shime amesema kuwa kikosi chake kitaibuka na ushindi
kutokana na vijana wake kuyafanyia kazi mafundisho yake anayowapa.
Mchezo huo utakaoanza saa 9.00 alasiri kwa saa za Afrika Kusini wakati huku
Tanzania itakuwa ni saa 10.00 jioni katika uwanja ambao hutumiwa na timu ya
Moroka Swallows.
Mchezo huo kwa Serengeti Boys utakuwa ni mtihani wa kwanza kati ya
miwili kabla ya kufuzu kuelekea Madagacar huku mchezo wa kwanza unafanyika
Afrika Kusini, kabla ya kurudiana Agosti 21 katika Uwanja wa Azam ulioko
Chamazi-nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment