Home Traders

Home Traders

Tembelea TK FM Redio 88.5 Tanga

Wednesday, 3 September 2014

Yajue MAPANGO YA AMBONI YALIYOPO TANGA

Na Kassim Discover
Naaaaaaaaaaaaaam Msomaji wa Tanga Kunani hakika ukiizungumzia Tanga basi imetimia na imezidi kubarikiwa bwana,haya tanga kunani yazidi kutukumbusha mengi kuhusu Tanga,na leo hii basi tunakuletea kivutio bora cha kitalii kilichopo ndani ya mkoa wa TANGA ambacho takribani watanzania walio wengi washawahi kusikia neno mapango ya Amboni ambayo kama hujawahi kusimuliwa na bibi/babu ama mtu wa karibu basi utakuwa umesoma ukiwa shule historia ya mapango haya ya Amboni jinsi yalivyokuwa maarufu na kuzidi kuutangaza mkoa wa Tanga vyema zaidi.
Yapo mengi sana ambayo naamini uliwahi kuyasikia,mimi binafsi nakumbuka wakati nakua kuna mtu alikuwa akitajwa na kuzungumzwa sana katika jamii yetu anaeitwa Salo Tango eti aliwahi kutafutwa sana bila mafanikio.
Dahhhhhhhhh kweli mapango ya Amboni yanaitangaza Tanga vyema sana,na istoshe pia niliwahi kusikia eti kuna Mzungu aliwahi kupotea na mbwa wake wakaonekana Mombasa huko KENYA,sasa nikajiuliza swali kichwani mwangu kuwa kumbe mapango haya yanafika mbali hivi?
Hizi ni mojawapo ya faida tunazojivuni wana Tanga
Naam msomaji wetu naamini kuna vitu hujawahi kuvisikia ndani ya mapango haya basi kabla sijakwambi vitu hivyo kwanza nataka nikufahamishe kuwa mapango ya Amboni yanapatikana mahali gani ndani ya Tanga?
Mapango ya Amboni yako katika eneo la Kiamoni, kata ya kiamoni, tarafa ya chumbageni, wilaya ya tanga.
Mapango haya yako umbali wa kilomita 8 toka tanga mjini kupitia barabara kuu inayoelekea Mombasa. Unaweza kufika katika hifadhi ya mapango kwa kupitia mojawapo ya njia zinazoelekea huko. Ya kwanza ni barabara ya changarawe iliyo upande wa kushoto meta 200 baada ya kuvuka daraja la Utofu, ya pili iko kilometa 1.5 kutoka daraja la utofu katika kituo cha ukaguzi wa mazao ya misitu. Njia zote zinapitia katikati ya kijiji cha kiamoni. 

Haya sasa wana Tanga na wale ambao sia wana Tanga kazi kwetu sasa kwa kukaribia Mapango ya Amboni kushuhudia mambo mengi na hata yale ya maajabu yaliyomo humo yakiwemo picha mbali mbali kama vile ramani za Afrika,michoro ya ndege,chui,Mengine ni pamoja na Bawa la ndege lililojichonga na kutengeneza picha halisi ya ndege ambayo unapoiona kabla hujasimuliwa waweza kuhisi ni ndege aliyefia ama kunasa mahala hapo siku za nyuma.
Pamoja na hayo pia kuna picha ya Mamba, Unyayo wa Tembo, Mlima Kilimanjaro, Mlango wa Ndege, Kochi lililojichonga,picha ya Chui iliyojichora juu ya mwamba na unyayo wa kiatu ila mwisho wa yote ni Njia nyembamba
pia kuna baadhi ya picha nyingine zilizojichora juu na pembeni mwa miamba kama Sanamu la Bikira Maria na Msikiti, ambavyo kila kimoja kimekaa upande wake na alama tosha za kuashiria kuwa ni picha uionayo mbele yako, huku msikiti ukiwa na badhi ya michoro inayoonekana kusomeka kama lugha ya  Quraan na kwa Bikira Maria kukiwa na alama ya kitabu kama biblia iliyofunuliwa na nyenginezo ambazo hizo zote zimejichora zenyewe bila kuchorwa.
Kwa kukuthibitishia hebu tazama hizi picha hapo chini.
Hebu tazama vizuri uone kama si chui huyu?
Mwamba ukiwa umejichora misili ya bawa la Ndege
Picha ya Simba ilivyojichora
Hya sasa msomaji wa Tanga Kunani ikumbukwe kuwa Mapango haya yametokana na mabadiliko ya nguvu za asili zilizobadilisha maumbile ya miamba ya chokaa kipindi cha jurasiki (Jurassic period) kama miaka inayosadikiwa kuwa zaidi ya milioni 150 iliyopita. Kulingana na tafiti zilizokwishafanywa, eneo hili la mapango lilikuwwa  chini ya maji miaka milioni 20 iliyopita na linakadiriwa kuwa na ukubwa wa kilometa za mraba 234 lenye mazingira ya miamba ya chokaa. Ni eneo ambalo linapitiwa na mito na limejaa uoto wa asili.
Miamba ya chokaaa kwa asili huundwa na madini ya kashiamu kabonate [ Calcium carbonate=CaCo3]. Miamba hii ni migumu kumomonyolewa na maji ya kawaida, lakini ni rahisi kuyeyushwa na maji yenye kiasi kidogo cha tindikali ya kaboni (Carbonic Acid). Tindikali ya kaboni iliyobadilisha maumbile ya miamba hii kwa kumomonyoa na kusababisha mapango yaweza kutokana na maji ya mvua yanapochanganyika na dioksidi ya kaboni (carbodioxide) hewani kabla ya kufika ardhini au na dioksidi ya kaboni inayopatikana ardhini. 
Haya ndio maajabu ya Amboni
Maji yanapojipenyeza ardhini huendelea kupokea dioksidi ya kaboni kutoka muozo wa viumbe hai kama mimea na wanyama na kutengeneza tindikali. Tindikali ya kaboni inapopambana na madini ya kashiamu kaboneti (calcium carbonate) katika miamba ya chokaa husababisha kumomonyoka kwa miamba hii katika maeneo mbalimbali na kusababisha mapango. Mabadiliko haya huitwa kabonesheni (carbonation). 


Msomaji wa Tanga Kunani haya sasa pia ningependa ufahamu kuwa
kulingana utafiti ulioishafanywa, umeonyesha kuwa miamba ya aina hii huongezeka kukua kwa kasi zaidi kipindi cha mvua kuliko kipindi cha kiangazi, na katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, ukuaji wake umekuwa milimeta 0.5 na kila baada ya miaka 100. na kuwa iliwahi kuongezeka kwa kasi ya milimeta 7 katika kila miaka 100 kipindi cha kati ya miaka 38000 na 34000 (38 & 34Ka).
Mwisho msomaji wetu ikumbukwe kuwa inasadikika kwamba   makabila ya Wazigua, Wambondei na Wasambaa walianza kufanya matambiko na kupata matibabu ya jadi. 
Sina la ziada kwaherini waungwana wa Tanga tukutane siu nyengine kwaheriiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
                               KARIBU SANA TANGA!

1 comment:

  1. Nilipotembelea Mapango ya Amboni mara ya mwisho nlikutana na magari kadhaa yakiwa na vikundi vya watu nilioamini walitoka kufanya Utalii wa Ndani kama sisi tulivyokuwa tunakwenda. Tulipofika tulikuta vikundi kadhaa na Wakati tunaondoka vingine vilikuwa Vinawasili. Hali hiyo inaonyesha kukubalika kwa Utalii huo wa ndani kwa Jamii ya Wanataanga na Majirani. Kuna haja kwa Halmashauri ya Jiji kulitilia hilo maanani na kuboresha huduma zipatikanazo Pembezoni mwa Mapango ya Amboni ikiwa ni pamoja na kuboresha barabara Inayochipukia barabara kuu ya Horohoro kuelekea Mapangoni.

    ReplyDelete