Home Traders

Home Traders

Tembelea TK FM Redio 88.5 Tanga

Tuesday, 2 September 2014

Ijue Tanga ilopangwa ikapangika

Na Kassim Discover
Naaaaaaaaaaam msomaji wa Tanga Kunani kama kawaidsa yangu basi nikiwa hapa tanga kunani hua nawasalimia waungwana wa TANGA kwa kumbushana vitu muhimu sana vinavyoihusu Tanga ama hata vile muhimu zaidi ya Tanga.
Wazee wetu
Kwanza mwana Tanga nataka ufahamu historia kuhusu Tanga.....
Kihistoria Mkoa wa Tanga ulitumiwa sana na wakoloni wa Kireno, Kiarabu, Kijerumani na Kiingereza ikiwa lango la biashara na uchumi kwa kuunganisha sehemu za ndani za Afrika Mashariki  na Kati na sehemu mbalimbali za Dunia kupitia bahari ya Hindi. Mwaka 1840 eneo  la  Manga  lilikuwa  njia  waliopitia wafanyabiashara  kutoka  Bara  Arabu  waliokuja kutafuta meno ya tembo  na  watumwa. 

Waarabu walikuwa wakiacha vyombo vya usafiri (majahazi) eneo la Sadani (Bagamoyo) na kuanza safari kupitia Manga, Kimbe hadi Kondoa Irangi. Misafara mingine ya  wafanyabiashara ilianzia Unguja kupitia Pangani, Kiwanda (Sindeni), Ngugwini, Mbego, Kwediboma, Mgera hadi Kondoa Irangi ambapo walileta nguo, shanga na vitu ili  kubadilishana  na  pembe  za ndovu, watumwa, chakula na mifungo. Kutokana na mwingiliano wa tamaduni mbalimbali, wenyeji wa Tanga wamerithi tamaduni, lugha na ustaarabu  wa mataifa  mbalimbali ya Washirazi, Waarabu,  Wachina, Wahindi, Wareno, Wajerumani, Waingereza na Waswahili.
Mkoa wa Tanga ni mzizi na chimbuko la Tanganyika kabla ya kuungana na visiwa vya Unguja na Pemba mwaka 1964 na kuunda Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Tanganyika ilipata Uhuru mwaka 1961 huku Mkoa wa Tanga ukiwa ni msafirishaji mkubwa wa zao la Mkonge  duniani  na  mhimili  wa  kukua kwa uchumi  wa  nchi.  
Jina  Tanga  lilitolewa  na wafanyabiashara  wa  Kishirazi  likiwa na maana  nne  ambazo  ni  Tambarare,  Mabonde  ya Kijani, Barabara za Milimani na Kilimo cha  Milimani. Neno nyika ni la kibantu ambalo lilikuwa likitumiwa sana na wenyeji wakimaanisha mbuga au pori zaidi ya jina Tanga.
Harakati za kudai Uhuru kutoka kwa wakoloni wa Kiingereza zilifanikiwa na Tanganyika kupata   Uhuru tarehe 9 Disemba, 1961 chini ya uongozi wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndani ya chama cha TANU. Wakati huo (1961) Mkoa wa Tanga ulikuwa ni Jimbo lenye Wilaya tano (5) ambazo ni Wilaya ya Tanga, Handeni, Pangani, Usambara na Same (Pare)
Haya sasa tuachane na hayo  leo msomaji wetu napenda tujuzane kwa ufupi tu kuhusu Tanga hebu nicheke kidogo  hahahahahahahaha yaani nikimaanisha nimefurahi sana kwani hakuna isieijua Tanga kua ni mkoa ulopangwa ukapangika bwana tena hebu nataka ufahamu kua hii wilaya ya wilaya usiseme jinsi ilivyopangwa ikapangika,tazama kuanzia mfumo wa barabara  daaaaa mpaka raha bwana yaani unaazia barabara ya kwanza hadi ishirini na moja tena kwa wale ambao hawafahamu kwa tanzania hii  mi najua ni mikoa miwili tu iliyokuwa na barabara za namba kama nitakuwa nimekosea basi msomaji wangu utanikumbusha kupitia kassimdiscover@gmail.com,naamanisha ni Tanga na Dodoma tena Dodoma yenyewe ina barabra chache kuliko Tanga hivyo basi lazima tujivunie kuwa wajerumani waliipanga tanga ikapangika.
Dala dala ya Mikanjuni
Ni mara chache sana mgeni kupotea akiwa ndani ya Tanga ikiwa ni mara yake ya kwanza kufika hapa dahhhhhhhh tuna kila sababu za kujivunia kua Tanga imepangwa ikapangika.
Stand ya mabasi
hahahahahahahah nazidi kucheka bwana hivi Tanga tuna kitu gani ambacho Mungu alitunyima jamani kuhusu viongozi usiseme nchi hii ukitaja uhuru wa nchi hii basi huwezi kusema hivi hivi bila kuwataja wazee wetu wa zamani ulivyotoa mchango wao katika kupigania uhuru wa nchi hii,soka usiseme,burudani kama vile sijui ngoma za asili,taarabu na nyinginezo hapa ndo palikuwa mahala kwake.
Watu mbali mbali walikuwa wakitoka Bara wakija Tanga kutafuta  maisha na wanafanikiwa na kwa ushahidi mpaka leo hii wengne tunao hapa hapa Tanga wameshindwa kabisa kurudi kwao na  familia zao zimezaa na zimeoa huku maisha yakiendelea kusonga mbele.
Ukarimu ndio usiseme bwana kwa watu wa Tanga yaani wanashulika katika shughuli mbali mbali za kijamii huku wakisaidiana katika raha na shida( harusi/maziko) watu wapo pamoja mwanzo mwisho.
Sio siri wengi  wana Tanga walizaliwa wakiwa ndani ya Barabara za namba zilizopangwa zikapangika na shule tulizosoma  zinajulikana bwana sijui Msambweni,Chuma,Masiwani,Mabawa na zile zilizokuwa zikitoa elimu kipindi hicho,,,,,,dahhhhhhhhh Tanga utaipenda bwana tulikuwa tukiumwa tu watu wanjiachia Ngamini kupata tiba huku tukiona kua kama vile Bombo ni mbali sana,haya usiseme watu walikuwa wanapenda sana kutumia soko flani hivi lina itwa soko mjinga kama mtakuwa mnalifahamu huku wakiliona kama vile soko kubwa la pale Ngamini au la pale Uzunguni nako kama vile mbaaaali vile lakini haya yote wana Tanga walikuwa wakiyatumia.
Soko la Ngamiani


 Waungwana wa Tanga mi bado nafurahi tu kuwa Tanga kwani wana TANGA kuna kamsemo kao wanapenda kukaita eti ukishindwa maisha TANGA huwezi kuyaweza sehemu kwengine daaaa sijui kamsemo haka ni cha kweli ama vipi,mhhhhh haya bwana lakini ki ukweli TANGA ya sasa pia inapendeza ina mandhari nzuri mjini yaani imepangwa kwa maua ya kupendeza kweli huku stand ya mabasi mpya ikijengwa pale maeneo ya Kange.
Mandhari Tanga ukishuka tu stand ya mabasi
Jamani ninayo mengi sana ya kuweza kuwajuza hebu kwa ufupi tu leo ni hayo kwa wenzangu wa Tanga ila kama unakumbuka chochote kile hebu unaweza kutoa maoni yako hapo chini ama tutumie email yako kuhusu TANGA.
Mi naondoka tutakutana siku zijazo chaooooooooooooooo!!!!
KARIBU TANGA

No comments:

Post a Comment