Home Traders

Home Traders

Tembelea TK FM Redio 88.5 Tanga

Wednesday, 3 August 2016

African Sports kutangaza kikosi chake kabla tarehe 6

Timu ya African asports ya jijini hapa inayoshiriki ligi daraja la kwanza inatarajiwa kutangaza kikosi chake kitakachoshiriki ligi daraja la kwanza kabla ya tarehe 6 mwezi huu.


Akizungumza na tk fm redio  leo mwenyekiti  wa African sports  Hatibu Heinz amesema kuwa   wakali hao wa zamani  bado wanaendelea na usajili na sasa wamebakisha wachezaji kumi na watasajili wachezaji takribani kumi na tatu ili kukiboresha kikosi hicho.

Aidha Henzi amesema kuwa mara baada ya kutangaza  wachezaji kikosi kinatarajiwa kuweka kambi daressalaam huku ikitarajiwa pia kutangaza ni mdhamini gani watakuwa nae.

No comments:

Post a Comment