Home Traders

Home Traders

Tembelea TK FM Redio 88.5 Tanga

Friday, 29 August 2014

Ronaldo azidi kutesa Ulaya,Mchezaji bora Uefa

 Hakuna asibisha kua mkali Ronaldo ni mkali mara baada ya kudhihisha ukali wake pale baada ya kutangazwa na Uefa kuwa mchezaji bora kwa kuwagaragaza kipa wa Bayern Munich, Manuel Neuer na Arjen Robben.
Mkali huyo aliisaidia sana timu yake ya Real Madrid kutwaa ndoo ya Uefa ametangazwa rasmi kube ndoo hiyo huku akizidi kuliwaza kundi la Uefa msimu huu baada ya kupangwa kundi moja na wakali wa Uingereza majogoo wa jiji Liverpool.
Cristano Ronaldo
 Licha ya kutangazwa kua mchezaji bora Ronaldo mwenye umri wa miaka 29 kwa sasa pia aliisaidia timu yake ya Real Madrid kutwaa kombe la Klabu Bingwa Ulaya - Uefa Champions League- msimu uliopita.
Ronaldo akiwa na jezi ya Madrid
Mwanandinga huyo kutoka Ureno alipachika takribani mabao 17  msimu uliopita na kuiwezesha wakali hao wa Hispania kutwaa ndoo hiyo.
Nikimnukuu mwanandinga huyo alisema kuwa alifurahi sana kutwaa tuzo hiyo lakini lazima niwashukuru  wachezaji wenzangu kwa sababu bila timu, tuzo binafsi ni vigumu kuzipata. 
Ronaldo akiwa ameshika tuzo yake
Ronaldo aliwazidi Neuer na Robben katika kura zilizopigwa na jopo la waandishi wa habari wapatao 54.
Neuer mwenye umri wa miaka 28, aliisaidia Ujerumani kushinda Kombe la Dunia, huku Robben mwenye umri wa miaka 30, akifunga magoli 21 ya Bayern na matatu kwa timu ya taifa ya Uholanzi iliyofika nusu fainali Brazil.
Ronaldo alifunga mabao matatu - hat-trick - wakati Ureno ilipoichapa Sweden katika mchezo wa kufuzu kucheza Kombe la Dunia, ingawa hakuweza kuwika Brazil, kwani Ureno ilitolewa katika ngazi ya makundi.
Ronaldo akiwa na jezi ya  Ureno

Lakini kikubwa kilichomsaidia Ronaldo kutwaa tuzi hiyo ni kiwango chake chake katika ngazi ya klabu ambacho kiliweza kushawishi jopo lililopiga kura, ambalo lilitakiwa kuchagua mshindi kati ya watatu hao baada ya mchujo kutoka wachezaji 10.
 Wakati huo huo Uefa pia ilitangaza viwango vya ubora kwa timu mbali mbali huku Real Madrid ikiongoza,Na hapa nakuletea kumi bora tu ya viwango hivyo:
              Timu            10/11            11/12            12/13       13/14       13/15      Points
1.Real Madrid CF33.642        36.171   29.542     39.600     4.642     143.599
2FC Barcelona36.64234.171    27.542     28.6004.642     131.599
3.Bayern München24.13333.050    36.585     29.9424.600     128.311
4.Chelsea FC26.67133.050    30.285     28.3574.628     122.992
5.SL Benfica25.76023.366    28.350     30.9834.550     113.009
6.Manchester United 36.67116.050        21.285    26.3570.628     100.992
7.Atlético de Madrid9.64234.171    13.542    37.6004.642      99.599
8.Valencia CF21.64225.171    22.542    26.6000.642      96.599
9.FC Schalke 0430.13320.050    22.585    18.9424.600      96.311
10.Arsenal FC22.67122.050    21.285     21.3574.628       91.992

No comments:

Post a Comment