SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limekabidhi mashine nne za
kufyatulia matofali kwa vijana 40 wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza ili
kusaidia wajasiliamali wadogo kupitia vikundi.
Akikabidhi mashine hizo ofisini kwake mwishoni mwa wiki, Meneja wa
NHC Mkoa wa Tanga, Isaya Mshamba kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Muheza, Ibrahimu Matovu alisema lengo la shirika hilo ni kuhakikisha
wanaisaidia serikali kupambana na wimbi la ukosefu wa ajira kwa vijana.
Alisema mpango uliopo kwa shirika hilo ni kugawa mashine hizo kwa
halmashauri zote za jiji la Tanga ambapo halmashauri zaidi ya nne
zimekabidhiwa, hivyo mashine hizo zitagawiwa
kulingana na vikundi husika.
kulingana na vikundi husika.
Matovu alilishukuru shirika la nyumba kwa jitihada za kupambana na
umasikini kwa kuwapa vijana mshine zitakazosaidia kuwapunguzia ukali wa
maisha.
Mwenyekiti wa kikundi cha Sarafina kilichopata moja ya mashine hizo, Shafii Ramadhani itawakomboa kiuchumi kwa kuongeza kiwango cha kazi zao.
No comments:
Post a Comment