Home Traders

Home Traders

Tembelea TK FM Redio 88.5 Tanga

Sunday, 23 November 2014

Kiporo chawatokea puani Villa Squad mbele ya African Sports

Mchezo wa kiporo kati ya African Sports ya Tanga na Villa Squad ya jijini Daresalaam hatimae umechezwa hapo jana katika uwanja wa Mkwakwani  na kuwafanya wana kimanu manu kukwea juu na kuzidi kuwafukuzia majimaji na Friends Rangers.
Hili lilikua ni goli la pili lililofungwa na Hassan Gurudum
Katika mchezo huo african Sports ya tanga ndio iliyotoka kifua mbele hadi kipenga cha mwisho kwa kuwabanjua villa mabao 2-1 huku Kocha mkuu wa timu ya villa Habibu Kondo akilalamikia maamuzi ya mwamuzi aliechezesha mchezo huo kwa ukdai kua aliwaua dhahiri shahiri kwa kuipendelea timu ya Africana Sports.
Akizungumza na TK Habibu Kondo amesema kua haiwezekani maamuzi haya na ndo maana ligi zetu na timu zetu siku zote haziwezi kua bora kwani kwa kitendo hiki zinapanda ligi kuu zikiwa bado hazina ubora wowote ambapo ni sawa na kuingia mlango wa mbele na kutokea wa nyuma yaani kama vile zinapanda daraja la manzese na kushukia uapande wa pili kwa kubebwa bebwa.
Kwa upande wa African Sports Alanus amesema kua mchezo ulikuwa mzuri  lakini yeye pia alishangazwa kwa maamuzi ya mwamuzi licha baadhi ya wachezaji hata kupigana viwiko.Aliendelea kusema kua wao kama Africana Sports watahakikisha wanarekebisha mapungufu yaliyojitokeza  na kikubwa ni kuhakikisha timu yao inapanda daraja hadi ligi kuu Bara.
Africana Sports kwa sasa imefikisha point 20 sawa na Lipuli ya Iringa yenye point kama hizo huku juu yao wakiwa frienda Rangers na majimaji ya songea wanaongoza majimaji wakiwa na point 24.

No comments:

Post a Comment