Home Traders

Home Traders

Tembelea TK FM Redio 88.5 Tanga

Friday, 29 July 2016

Mo Dewj Afunguka atangaza Billioni 20 kuwekeza Simba

Mkereketwa  mkuu na mwanachama  wa timu ya Simba Mohammed Dewji amesema kuwa  angependa kuwekeza Simba ili kubadili mfumo wa timu hiyo.

MO DEWJ
  Akizungumza na  waandishi wa habari  leo jijini Dar es Salaam Mo amesema kuwa  bajeti ya Yanga na ile ya Azam FC ni mara mbili ya ile ya Simba, jambo linaloifanya klabu hiyo kuendelea kubaki kuwa msindikizaji.

Tayari Mo amesema yuko tayari kutoa Sh bilioni 20 ili kununua hisa asilimia 51 na kuwekeza ndani ya Simba na atafanya hayo iwapo Simba SC watakubali kumuuzia asilimia 51 ya hisa kwa Sh. Bilioni 20.

“Nipo tayari kuwekeza Bilioni 20 kama watanipa nafasi lakini tukubaliane kuwa hakuna mtu atagusa pesa hizo , tutauza bondi na kwa kila mwaka tutaingiza Bilioni 3.5 na tutatengeneza mapato ya Bilioni 2 kila mwaka ukijumlisha ni Bilioni 5.5 ambayo itakuwa ni bajeti ya mwaka,

“Inaniuma sana kuona klabu imekuja juzi tu leo inatuzidi mafanikio lakini kama Yanga na Azam bajeti zao kwa mwaka ni Bilioni 2.5 hadi Bilioni 3, sisi tukiwa na bajeti ya Bilioni 5.5 tutakuwa tumewazidi na tutaleta wachezaji wazuri na kocha mzuri,” alisema na kuongeza.

Aidha Mo amesema kuwa kama akiuziwa asilimia 51 ya hisa na kuwa mmiliki wa Simba, atawawezesha wanachama wa muda mrefu wa klabu hiyo kupewa hisa bure, ambazo wataamua wenyewe kuuza, au kununua hisa zaidi.
Mo Pia amesema kuwa  mafanikio kwenye mpira, hakuna zaidi ya fedha hivyo Simba haiwezi kuwa na miaka 80 leo haina hata uwanja wa mazoezi hakika inaniuma.
"Mimi ninaamini Simba haiwezi kubadilika kwa kuwekeza kwenye bajeti ya Sh milioni 500 kwa mwaka. Haitawezekana, ndiyo maana nimekuwa nikisisitiza, kwanza Simba inahitaji muwekezaji na si mdhamini.

“Shabaha yangu ni kuitoa klabu kwenye Bajeti ya Bilioni 1.2 hadi Bilioni 5.5, mashabiki wa Simba wanahitaji mafanikio ya haraka, lazima tusajili vizuri, tuajiri kocha mzuri. Ukitenga Bilioni 4 kwa mwaka, tayari umewazidi wapinzani Azam na Yanga,”.

Amesema lengo lake ni kuifanya Simba itwae ubingwa wa Afrika kwa kushindana na timu kama TP Mazembe zinazotumia Bajeti ya Sh. Bilioni 20 kwa mwaka.


No comments:

Post a Comment