Mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri na Uteuzi wa Naibu Waziri.(Martha Magessa)

Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dr Mohamed Ally Shein
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed
Shein amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri na pia
kumteuwa Naibu Waziri kama ifuatavyo-

(a) Mhe.
Dkt. Sira Ubwa Mamboya ameteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo na Maliasili
akijaza nafasi ilioachwa wazi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Mhe.
Suleiman Othman Nyanga.
(b) Mhe.
Juma Duni Haji ameteuliwa kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano
akichukuwa nafasi ilioachwa wazi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Mhe.
Rashid Seif Suleiman ambaye sasa anakuwa Waziri wa Afya.
(c) Mhe.
Rashid Seif Suleiman ameteuliwa kuwa Waziri wa Afya akijaza nafasi ya
Mhe. Juma Duni Haji ambaye sasa anakuwa Waziri wa Miundombinu na
Mawasiliano.
(d) Mhe.
Mahamoud Thabit Kombo ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Afya akijaza
nafasi ilioachwa wazi na Mhe. Dkt. Sira Ubwa Mamboya ambaye ameteuliwa
kuwa Waziri wa Kilimo na Maliasili.
Na pia amefanya mabadiliko ya baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya.
Aidha,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali
Mohamed Shein amefanya mabadiliko ya baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya
kama ifuatavyo:-
(1).
Major Mstaafu Juma Kassim Tindwa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa Kaskazini
Unguja akijaza nafasi ilioachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Bwana
Pembe Juma Khamis.
(2). Bibi
Mwajuma Majid Abdulla ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa Kusini, Pemba
akijaza nafasi ilioachwa wazi na Major Mstaafu Juma Kassim Tindwa ambaye
amehamishiwa Mkoa Kaskazini, Unguja.
(3).
Bwana Omar Khamis Othman ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini,
Pemba akijaza nafasi ilioachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Bwa.
Dadi Faki Dadi.
(4).
Bwana Ayoub Mohamed Mahmoud ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi
akijaza nafasi ilioachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Bwa.
Hassan Mussa Takrima.
(5). Bibi
Hanuna Masoud Ibrahim ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake
akijaza nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Bibi Mwanajuma Majid
Abdulla ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa Kusini, Pemba. Utezi huo
umeanza Jana tarehe 24 Agosti 2014.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment