Ugonjwa w Ebola hakuna asieusikia jinsi unavyotesa wanadamu na kuua kwa dakika chache sana,kufuatia hayo sasa Serikali ya Tanga ulitenga vituo vikuu vitatu vya Afya ikiwa ni hatua ya maandalizi ya kudhibiti watu wataobainika kuambukizwa virusi vya homa hiyo ya Ebola
Tukiwa kama Tanga Kunani leo hii ni bora mkazi wa Tanga uvifahamu vituo hivyo kwa manufaa yetu kwa pamoja,Mkuu wa mkoa wa Tanga Chiku Gallawa aliwahi kubainisha siku chache zilizopita kuwa vituo hivyo ni kile cha mpaka wa Horohoro wilayani Mkinga, Masiwani Shamba
na Maramba.
Alisema
kuwa timu maalumu ya mkoa ya wataalamu wa afya, tayari inakagua uwezo wa
vituo vingine vilivyotengwa na halmashauri nyingine za mkoa huo, kama
vinastahili kupokea wagonjwa wa aina hiyo.
Alisema
ingawa mpaka sasa hakuna mgonjwa wa ebola nchini, serikali imechukua
hadhari hiyo, kuwaondoa wasiwasi wananchi kutokana na mwingiliano wa
wageni kutoka nchi jirani kupitia mpaka wa Horohoro.
Alisema
vituo hivyo vitatu vimeimarishwa kwa kupelekewa vifaa tiba, madaktari
na wauguzi wenye stadi za kutosha na vitatumika kutoa huduma kwa
wagonjwa watakaobainika.
No comments:
Post a Comment