Kampuni ya Sony hatimae umeufunga Mtandao wa Sony Playstation kufuatia hofu ya kushambuliwa kwa mtandao wake wa kutoa huduma ya playstation.
Katika ujumbe kwenye mtandao wake , Sony imesema kuwa hakuna habari za watu binafsi zilizohatarishwa kufuatia shambulizi hilo.
Siku ya jana "Jumapili"ndege aliyokuwa akisafiria
mmojawapo wa maafisa wakuu wa Sony, ililazimika kubadilisha mkondo
kufuatia hofu ya kulipuliwa.
Baadaye ilibainika kuwa kundi linalodai
kutekeleza shambulizi hilo la mtandao, kupitia kwa mtandao wa kijamii wa
Twitter uliashiria kuwepo kwa tishio la usalama kwa ndege hiyo.
Katika taarifa hiyo Sony ilisema kuwa
“mtandao wa Playstation na mtandao wa burudani wa Sony iliathirika
kufuatia jaribio la kufululizia tovuti zao watumiaji wengi na kuizuia
kutoa huduma hata hivyo kampuni hiyo imesema kuwa itajitahidi kusuluhisha swala hili na wanaamini kuwa kuwa hali ya huduma zake itarejea haraka iwezekanavyo.
Hata hivyo Sony imesema kuwa wapelelezi wa FBI
wanachunguza tishio la usalama kwa ndege aliyokuwa akisafiria rais wa
Burudani ya Sony Mtandaoni John Smedley, ambayo ilitarajiwa kutua San
Diego lakini ikalazimika kubadilisha mkondo na kutua Phoenix, Arizona.
Mtandao huo wa sony wenye zaidi ya wateja
milioni 52 wa Sony Playstation umewahi kushambuliwa na wavamizi wa
mtandaoni hapo awali, likiwemo shambulizi lililoiba habari za siri za
mtandao huo, mwaka 2011.
Hii leo Sony inatarajiwa kurekebisha usalama wa mtandao huo ambao hufanyika mara kwa mara kwa mtandao wake wa PlayStation.
Baada ya 1740 BST, huduma fulani zikiwemo
duka la PlayStation, akaunti ya usimamizi na usajili ya PSN, huduma za
burudani na michezo ya mtandaoni hazitakuwepo, kwa sababu ya
marekebisho.
No comments:
Post a Comment