Kutokana na hali hiyo, Chadema imedai kubaini uwepo wa mamluki hao
ambao wengi wamejitokeza kuwania nafasi mbalimbali katika chama hicho
huku wakikosa sifa stahili na hata kupanga mikakati ya kwenda mahakamani
kupinga uchaguzi huo pindi majina yao yatakapokatwa kwa kukosa sifa.
Kwa mujibu wa chanzo cha habri hii gazeti li mtanzania ni kuwa

Kwa mujibu wa kanuni za Bavicha, mgombea yeyote anatakiwa kumaliza
kipindi cha uongozi wake kama atachaguliwa akiwa na umri wa ujana ambao
kwa kanuni za baraza zinasema asizidi miaka 35 pindi awapo madarakani.
Kanuni hizo zinafafanua kwamba, ni lazima mgombea yeyote asiwe amezidi umri wa miaka 30 wakati anagombea.
Kutokana na mvurugano huo, taarifa kutoka ndani ya Chadema zinaeleza
baadhi ya wanachama waliochukua fomu wengi wao wanazijua sheria na
kanuni za chama hali iliyosababisha kuzusha maswali miongoni mwao.
Katika uchunguzi uliofanywa kwa baadhi ya wanachama wanaowania nafasi
hizo umebaini wengine wakiwa na umri ulio juu ya miaka ya kanuni ambayo
ni 18-30.
Mmoja wa waliochukua fomu za kuwania uongozi ndani ya Bavicha ambaye
hakuwa tayari kutajwa jina lake, amesema kuwa kanuni
alizotumia kuwania uongozi wa vijana ni za chama ambazo zinasema
waziwazi kwamba umri wa ujana ni hadi miaka 35.
“Sidhani kama nina kosa kutumia haki yangu kuwania nafasi hiyo, kwa
sababu naamini kwa mujibu wa kanuni za chama zinaonyesha wazi kwamba mtu
mwenye miaka 35 bado ni kijana, kwa kuwa nina miaka 31 sioni kosa kwa
kuwa bado ni kijana.”
Chanzo caha habari hii yaani gazeti la mtanzania lilipofuatilia kwa undani ni kitu gani kinachowafanya
baadhi ya makada hao kuweka mikakati ya kwenda mahakamani kuzui uchaguzi
huo, baadhi yao walisema hivi sasa kuna mgongano wa kisheria kati ya
kanuni za uchaguzi na katiba ya Chadema.
Baada ya kubainika mipango hiyo, Chadema imetoa maelekezo kwa
viongozi wa vijana na wanawake kuhakikisha kila fomu ya mgombea inakuwa
na vielelezo muhimu ikiwemo cheti cha kuzaliwa.
Kauli ya Chadema
Akizungumzia kuhusu mikakati hiyo, Mkurugenzi wa Oganaizesheni
Uratibu wa Kanda, Singo Kigaira Benson, alisema suala la umri wa kijana
uko wazi kwani kanuni zimekuwa zikisema sifa ya mtu anayestahili
kugombea uongozi.
“Kanuni zinaposema mtu anayefaa kugombea ni yule ambaye hajazidi
miaka 30, isichukuliwe kuwa ni maneno ya mtu yanayotoka kinywani, kama
hao mamluki hawazijui kanuni za chama wasome. Na kama yupo anayejiingiza
kugombea huku akijua umri wake umezidi na baadaye kwenda mahakamani
atakuwa anajidanganya,” alisema.
Kigaila aliongeza kuwa chama hakitamvumilia yeyote atakayedanganya umri, ataadhibiwa kwa kutumia kanuni za chama.
Alisema: “Hiyo haiwezi kuwa sababu ya kufutwa kwa uchaguzi na wala
uchaguzi wa Chadema haufutwi na mahakama bali unapingwa ndani ya vikao
halali vya chama na hata mamluki wanapokuja wahakikishe wamejipanga,”
alisema.
Alisema kuwa chama hicho kimeongeza muda wa kuchukua na kurudisha
fomu kwa siku tano kutoka Agosti 25 na sasa utakuwa Agosti 30, mwaka huu
saa kumi jioni.
Alisema kuwa sababu ya kusogeza mbele ilichangiwa na wingi wa maombi
kutoka kwa wanachama mikoani wakitaka usogezwe ili waweze kumalizia
uchaguzi wa ngazi za mikoa na kupata fursa pana ya kushiriki uchaguzi wa
kitaifa.
Peneza ajigamba
Kwa upande wake mgombea wa nafasi ya Uenyekiti katika Baraza la
Vijana wa Chadema (BAVICHA), Upendo Peneza, amesema chama chake
hakikumtuma kugombea nafasi hiyo isipokuwa dhamira ya kuleta mabadiliko
ndani ya chama na Taifa ndiyo vimemsukuma.
Upendo ni kijana wa kwanza mwanamke kugombea wadhifa huo ndani ya Bavicha.
Alisema kitu cha kwanza atakachokifanya endapo atafanikiwa kushika
cheo hicho ni kuweka msisitizo katika ajenda za vijana ndani ya chama
pamoja na taifa, ikiwemo ubora wa elimu iliyo sawa kwa wote pamoja na
ajira za kudumu.
“Leo natangaza dhamira yangu ya kugombea nafasi ya uenyekiti katika
Baraza la Vijana Chadema, kwani nimeshachukua fomu na kesho (leo)
natarajia kuirudisha.
“Kikubwa kilichonisukuma kuchukua uamuzi huu ni nia yangu ya dhati
kabisa ya kuleta mabadiliko ndani ya Bavicha na kwa vijana wote wa
Tanzania bila kujali tofauti ya dini, kabila au vyama,” alisema Upendo.Chanzo Mtanzania
No comments:
Post a Comment