Bomu linalodhaniwa kutupwa kwa mkono na majambazi kutoka nchi jirani ya Burundi hatimae sasa limesababisha watu takribani wanne kufariki dunia hadi sasa,majeruhi Regina Mzakule (66) amefariki dunia na kufanya idadi ya
waliokufa katika tukio la bomu la kutupa kwa mkono ndani ya gari la
abiria wilayani Buhigwe, Kigoma kufikia wanne.
Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kasulu,
Joshua Monge alisema alipokea majeruhi saba wa tukio hilo akiwemo
marehemu huyo.
Alisema marehemu huyo alipata majeraha makubwa na vipande vya chuma kumuingia tumboni.
Aliwataja majeruhi watatu walioruhusiwa kuwa ni Honolina Benjamini
(42), Kabula Matius (40) na Agripina Jeremia (45) wakati wanaoendelea na
matibabu ni Shukrani David (32), Tedy Charles (25) na Osward Samweli.
No comments:
Post a Comment