Tembelea TK FM Redio 88.5 Tanga
Khalid Rashi aimwaga Chadema na kujiunga na ACT-Tanzania
Katibu wa Wilaya ya
Tanga Chadema Khalid Rashid amejiudhulu wadhifa wake na kujiunga na chama cha Alliance
for Change and Transparence (ACT-Tanzania) pamoja na wajumbe tisa wa kamati ya utendaji.Katibu huyo alijivua nyadhifa hizo sambamba kabisa na Husna Mawe wa Baraza la Wanawake Chadema
(Bawacha). Wajumbe waliojiuzulu toka chama hicho ni Hussein Baruti, Mohamed
Kidege, Hassan Maulid, Juma Yunusi, Zaina Manyeki, Seleman Hassan,
Mwanaisha Kambimbaya, Mohamed Sululu na Kisua Mrami Kisua ambaye pia ni
mweka hazina.Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari
jana, Rashid amedai kuwa sababu za kujitoa zimetokana na kuandikiwa
barua ya kusimamishwa uongozi kinyume cha katiba huku akipewa tuhuma
kumi zisizo na ukweli.Miongoni mwa tuhuma hizo ni kupingana na maelekezo
ya kamati kuu kuhusu kumvua nyadhifa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa
Chadema, Zitto Kabwe. Sababu nyingine ni namna uongozi taifa
ulivyoshughulikia suala lake kishabiki bila kufuata taratibu.
No comments:
Post a Comment