Home Traders

Home Traders

Tembelea TK FM Redio 88.5 Tanga

Wednesday, 27 August 2014

Mgosi Kibaja"NAWAKAZIA"

Na Kassim Discover
Kama kuna mtu anaekuja kwa kasi katika tasnia nzima ya Hip Hop Hapa nchini na hapa mkoani Tanga ni jamaa anaejulikana kama MGOSI KIBAJA/KIBAJA MGOSI,ambae kwa sasa anafanya poa sana katika tasnia ya muziki mara baada ya kuachia mzigo wake wa pili unaojulikana kwa jina la Nawakazia.

Kama utapata fursa ya kukutana nae huyu jamaa basi utakua unamfahamu kwani ni mwana Tanga aliekulia mikononi mwa wana Tanga na Anaetoka katika famiuliya ya Mpira ya Kina James Kisaka.
Haya sasa tuachane na hayo mimi binafsi jamaa sikutegemea kama atajikita huku lakini ukweli halisi ni kuwa jamaa anaweza bwana kama ni mfatiliaji mzuri hebu sikiliza ule mzigo wake wa kwanza unaojulikana kwan jina la AMSHA AMSHA aliowahi kumshirikisha swahiba wake ROMA MKATOLIKI alafu utajijibu kua ni mkali tena mbayaaaaaaaaa!

Unapolizungumzia gemu la Hip Hop Tanzania hii basi hutosita kumtaja mkali ROMA ambae ameitangaza vema kweli mkoa wa Tanga kwa ngoma zake kali zinazotoa ujumbe mkali huku zikitoa kama tongo tongo kwa wale wenye matongo tongo,lakini si sehemu yetu kwa leo kwani nilikuwa napita tu hapo ili ufahamu kuwa Tanga wapo wakali bwana.
Mgosi Kibaja Kwa wale walibahatika kusoma shule ya Msingi Masiwani na Mkwakwani Sekondari basi watamkumbuka vema kwa kipaji chake cha kusakata mpira huku akiwa mnazi mkubwa wa wana jangwani YOUNG AFRICAN lakini si hivyo,kwa sasa jamaa kajikita  zaidi katika tasnia ya Muziki.

Kikubwa na swali la msingi la kujiuliza mwana Tanga,mgosi Kibaja kufaata nyayo za Roma!!Sapoti kubwa wana Tanga inahitajika kwa vijana wetu kama hawa kwani kazi nzuri husapotiwa bwana,Mimi nasepa namna hii kwa kuachia mzigo wa wake.BOFYA HAPA KUSIKILIZA NAWAKAZIA

No comments:

Post a Comment