Kama kuna wimbo unaofanya vizuri kwa sasa katika vituo vya Redio Tanzania hii na hasa hapa mkoni Tanga ni wimbo wa kwake Lina,mwanadada alietokea pale katika nyumba ya vipaji ya Tanzania House of Talent (THT).
![]() |
Lina Akiwajibika Jukwaani |
Mwana dada huyu alifyatua kabao chake hicho si muda mrefu lakini kwa sasa kinasumbua kweli katika vituo vya Redio hapa Tanga na istoshe pia aliitendea haki ngoma hiyo pale katika shangwe za FIESTA hapa Tanga baada ya washabiki kulipukwa na shangwe baada ya kuanza kuiimba ngoma hiyo.
Licha ya kufanya poa kwa sana katika vituo vya Redio lakini pia ngoma hiyo inaoongoza kusikilizwa katika mitandao ya kijamii na KUDOWNLODIWA hususani katika mtandao wa HULKSHARE wa Kipindi cha Planet.
Kama utapata fursa ya kuisikiliza ngoma hii basi lazima utaipenda kuanzia mahadhi yake jinsi ilivyopangiliwa ikapangika huku ikizungumzia zaidi kuhusu mapenzi.
Kuthibitisha hili wala usipate tabu hebu Bofya hapa
No comments:
Post a Comment