Home Traders

Home Traders

Tembelea TK FM Redio 88.5 Tanga

Thursday, 28 August 2014

Makala ya Leo!!!Ufahamu Ugonjwa wa Ebola

Na Kassim Discover
Naaaaaaaaaaaaaaaaaaaam Msomaji wa Tanga Kunani sasa leo tunakuletea ugonjwa hatari sana wa Ebola ambao unaua na unazidi kuua barani Afrika na istoshe ugonjwa huu sasa umekua tishio kweli huku Afrika Mashariki wakijilinda kukabiliana nao ugonjwa huu.
Wadudu wa ugonjwa wa Ebola

Msomaji wa Tanga Kunani hivi unajua ni kwanini ugonjwa huu uliitwa Ebola?Haya sasa tanga kunani inakupasha kuwa uliitwa ebola kwasababu uligundulika katika mto Ebola Mnamo mwaka 1976 ambalpo ndipo ulipopata jina hili,huku wataalamu wakizidi kusema kusema kuwa ugonjwa huu uligundulika nchi za Sudan na Congo.
Mgonjwa mwenye Dalili za Ebola

 Sasa Ugonjwa huu kwa mujibu wa madaktari mbali mbali umeua pia jamhuri ya Congo huku nchi jirani kama vile ukanda huu wa Afrika Mashariki wakijaribu kuweka vituo mbali mbali mipakani ili kuzuia ugonjwa huu kwa wale wagonjwa watakaobanika kuambukizwa ugonjwa huu.

Ikumbukwe kua si ugonjwa wa hatari wala mchezo kwani hata hao madaktari pia umewaua,lakini hadi sasa ukikadiriwa kuua zaidi ya asilimia 88 ya watu.

Msomaji wa Tanga Kunani kwa mujibu wa wataalamu inasadikiwa kua ugonjwa huu unasababishwa na homa ya ubongo huku ukidaiwa kujulikana kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1976 katika bara la Afrika,huku watu wapatao takribani 1200 wakisadikiwa kufariki kwa ugonjwa huu wa ebola kati ya 3147.
Madaktari wakimpa tiba mwathirika wa Ebola

Istoshe msomaji wa Tanga Kunani ugonjwa huu una dalili zake ambazo kwa mjibu wa madaktari wanasema kua kati ya siki 2 hadi 21 hujitokeza mara baada ya maambukizi lakini zaidi kabisa kati ya siki 8 hadi 10.Hata hivyo dalili hizi kuenda sambamba kabisa na mafua,homa kali,Uchovu wa ndani ya mwili, Misuli kuuma.Kuumwa kwa Kichwa pamoja na Koo kuvimba.

Hata hivyo kwa mujibu wa hao hao madaktari ni kuwa mara baada ya mgonjwa kupata dalili hizo hapo juu,baadae mgonjwa huanza kuharisha,kutapika,upele mwili,ufanyaji kazi wa figo pamoja na Ini hua ni mdogo sana,inadaiwa pia damu huvuja ndani ya mwili na hata kutokwa na damu sehemu zote zenye tundu katika mwil.


Sasa msomaji wa Tanga Kunani hebu nikupe taarifa fupi tu kuhusu usambaaji wake,ni kuwa ugonjwa huu usambaaji wake unaweza kusambazwa toka kwa  wanyama kama nyani na hata kwa binadamu kwa  kugusa damu ilioathirika au majimaji ama kidonda. 
Naamini sasa Tanga Kunani imekupa ladha na kukuhabarisha kuhusu ugonjwa huu hatari wa Ebola,tukutane siku nyengine katika makala nyengine.

 
 

 


No comments:

Post a Comment