Home Traders

Home Traders

Tembelea TK FM Redio 88.5 Tanga

Saturday, 23 August 2014

Sports

Mrwanda amtaka Malinzi kuacha utani
 Mshambuliaji wa zamani wa wekundu wa msimbazi Simba na anaecheza soka la kulipwa nchini Vietnam kwa sasa akikipiga katika timu ya Polisi ya Morogoro Danny Mrwanda amemtaka Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, kuacha utani juu ya timu ya taifa kwa kuangalia kikosi cha timu ya Maboresho.
.Hata hivyo, licha ya jopo la makocha kukaa na kuwapata wachezaji hao na kuwaweka pamoja na wazoefu kambini,lakini kocha wa Stars, Mart Nooij aliwapukutisha wote katika kikosi chake kwa madai bado hawajamshawishi, ingawa baadhi ya wachezaji hao wamechukuliwa na klabu mbalimbali za Ligi Kuu.
Mrwanda,alisema kuwa  kwa hilo Malinzi amefanya ‘utani’ kwani hakuna nchi yoyote duniani inayowatumia wachezaji ambao hawana klabu kwenye timu zao za Taifa.
“Mimi siungani na Malinzi katika hilo, kwani nilifikiri labda wale wachezaji wa maboresho wangewekwa kwenye Academy, wangefundishwa hapo na kutafutiwa klabu mbalimbali za ligi ili kuwapa uzoefu na ndipo wajumuishwe katika timu ya Taifa, lakini naona wao wanataka wacheze moja kwa moja Stars hilo jambo limenishangaza na wala sijawahi kuona kokote.
“Hakuna Timu ya Taifa yoyote duniani inayotumia mchezaji ambaye hana klabu, ndio kwanza tungeanza sisi, hilo jambo haliwezekani na nalipinga, nafikiri waliokuwa wamefikiria wamekosea na wanatakiwa kujipanga upya,” alisemaMrwandwa.

Wakati huo huo, Chama cha soka nchini Tanzania TFF hatimae kimerejesha tena mashindano ya FA CUP, ambayo kwa sasa yanajulikana kama federation Cup.
Mashindano hayo  yanatarajiwa kuanza Mwezi Novemba Mwaka hu huku yakitarajiwa kushirikisha
timu zote zilizosajiliwa Nchini na ambazo zitaomba kushiriki na Droo yake haitabagua Timu za Madaraja tofauti katika upangaji Mechi zake za Mtoano.

Mechi za FA CUP zitachezwa katikati ya Wiki na Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kwa Msimu mpya wa 2014/15 imetambua hili kwa kupanga Mechi zake za Ligi Wikiendi tu.

Kwa mujibu wa habari toka TFF, Mashindano haya yatapewa msaada na FIFA na pia inatarajiwa Wadhamini mbalimbali wa ndani ya Nchi watashiriki kuyafadhili.


Habari Mbali Mbali zaKimichezo za  Kimataifa

Kusajiliwa kwa Mario Balotel Liverpool ni Majanga-Jamie Redknapp...

Huku timu ya liverpool ikifanikiwa kumsajili mchezaji wa zamani wa man city Mario Balotel Nahodha wa  zamani wa Liverpool Jamie Redknapp amedai kuwa kusajiliwa kwa mchezaji huyo kutaivuruga timu hiyo.






 
 
 
 
 
 
 
 Asmir Hauzwi-Hughes
 Meneja wa timu ya Stock City Mark  Hughes amesema kuwa mlind mlango wake Asmir Begovic  hatoondoka katika timu hiyo katika dirisha hili la usajili.
Kufuatia kutolewa kwa kauli hiyo sasa na bosi huyo kunaiweka liverpool,Manchester city na Arsenal midomo wazi na kushaanga hewani kutokana na kumuwinda mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 27 kwa sasa,huku timu hiyo ya Stock ikisema kuwa bado haijapokea ofa yoyote toka kwa  timu zinazomuwania mlinda mlango huyo.



Howard kustaafu soka 2018.
Mlinda mlango wa timu ya everton ya nchini uingereza Tim Howard hatimae amefikiria kustaafu soka lake ifikiapo  mwishoni mwa kombe la dunia la mwaka 2018.
Golikipa huyo amesema kuwa ifikapo mwaka huo itakuwa amemaliza mkataba na timu yake ya Everton hivyo ndio itakuwa mwisho wa soka kwake


            

No comments:

Post a Comment