Home Traders

Home Traders

Tembelea TK FM Redio 88.5 Tanga

Monday, 25 August 2014

Makala ya Leo!


Mauza uza ya hospitali ya Bombo
Na Kassim Discover
Msomaji wa Blog hii ya  tanga Kunani   wakati naianza safari  yangu ya  kuianda makala hii ilikuwa ni muda wa usiku ndipo kila nikizidi kwendambele zaidi nahisi kama woga flani hivi  kwa jinsi mauza uza haya yalivyomtokea msimamizi wa chumba cha maiti hospitali ya Bombo huku nikijiuliza swali je,kama mimi au wewe unatokewa na hali kama hizi dahhhhhhhhhh weeeeeeeeeee lazima kivumbi kingetokea na mengi yangesemwa tu!
Jengo  la chumba cha kuhifadhia Maiti katika Hospitali ya Bombo
Musa Hamadi  ni mtumishi  katika Hospitali ya Bombo Tanga  chumba cha kuhifadhia maiti  yaaani mochwari,Bwana Musa Hamadi aliianza kazi katika chumba cha maiti  mnamo tarehe  8/9/1981 hadi wakati huu licha ya kukutana na changamoto na mauza uza mbali mbali katika kazi hiyo ambayo yamempa ujasiri wa hali ya juu na kuzidi kuizoea kazi yake hiyo, kazi yake kubwa  hapo ni kuhifadhi maiti ambazo zimetoka wodini ama nyumbani kwa heshima zote kwa kuiweka sehemu nzuri katika jokofu zake za kuhifadhia  maiti hiyo mpaka pale ndugu wa marehemu   watakapofatilia maiti yao kwa ajili ya mazishi ndipo huwakabidhi wahusika.
 Kwa wale wanaofatilia maiti zao huwa wakifika mochwari humtajia jina la maiti huyo ambapo yeye kama muhusika kwa uzoefu wake huwa anaingia katika chumba cha maiti  na kuwatolea ama kuwaonesha wahusika maiti zao ambazo huifadhiwa katika majokofu huku kila jokofu likiwa na jina la marehemu na huku wakitakiwa wawe na kibali kutoka katika wodi aliyofika marehemu yaani ‘’Death Certificate’’.
Bwana Hamadi ni  hodari sana katika kuzifanyia uchunguzi maiti ambazo bado hazijafanyiwa ucgunguzi aidha zilizopelekwa hapo na jeshi la polisi ambazo bado hazijafanyiwa,ambapo ujuzi na utaalamu huo ameupata hapo hapo hospitali ya Bombo na kule mjini Morogoro alikokwenda katika semina ya uchunguzi, zaidi  akimshukuru  marehemu Dokta Muhina aliekuwa Daktari katika hospitali hiyo  kwa kumfundisha kazi hii ya uchunguzi yaani ‘’Prosmoter Investigation’’.

 Kama nilivyokwambia hapo awali mpenzi msomaji wa Tanga Kunani  kuwa wakati naiandaa makala hii hali flani ilinijia kama hofu flani hivi kutokana na kusisimua kwake na sasa hebu nifatilie kwa makini sasa ufahamu mauzaza hayo ya ya Mochwari.

Kuna mauzauza ya aina mbili ambayo msimamizi au mtumishi wa mochwari Ndugu Musa Hamadi aliwahi kukutana nayo miaka hiyo ya nyuma ni kuwa mnamo mwaka 1988 mida ya saa saba za mchana  akiwa ofisi kwake amejipumzisha alisikia ghafla mlango ukifunguliwa kwa kasi ya ajabu huku watu wakitembea  huku  zikitoka sauti kama za mtu au watu waliovaa viatu vya kokoko,alishangaa sana akajiuliza ni nani walioingia humu ndani bila ya mimi kuwaruhusu au ni kina nani wanaoosha maiti bila ruhusa yangu? Akajipa moyo zaidi ikamlazimu afatilie   ndani ili awajue ni kina nani hao walioingia bila taarifa lakini cha kushangaza hadi alipofika mlangoni alikuta mlango umefungwa kama ulivyo na hakukuwa na ishara yoyote ile ya mlango kama umefunguliwa ama kufungwa,alishangaa sana  kuona hivi akarudi zake kupumzika lakini mara baada ya muda mchache  kupita  hivi akasikia  upepo mkali unavuma ndani,akaingia tena hadi ndani hakukuta mtu wala kitu chochoe kile lakini alijipa moyo zaidi kwa kuwa wapo karibu na bahari labda ni mambo ya majini jinni tu huku  mwenyewe hakikataa kuamiani  kama kweli yapo.Licha ya Ndugu Hamadi kukutana na mauzauza mengi siku nyengine alikuwa akiwa amekaa ikaja pickup nyeupe ikiwa na watu kama sita hivi akiwemo dereva pamoja na watu wengine waliomo yaani kama vile wanakuja kuchukua maiti walikuja wakaelekea moja kwa moja hadi upande wa nyuima wa mochwari,ndipo Bwana Hamadi    ikabidi awafate  labda inaweza ikawa hawa watu ni  wageni hawaelewi mlango wa kwenda kuchukulia maiti ni upi lakini pia cha kushangaza na cha ajabu  alizunguka mochwari kama mara mbili hakuona gari wala mtu yoyote wala dalili ya mtu kwenda huku akijiuliza bila kupata majibu asijue ni wapi walipokwenda watu wale walokuja.

Mpenzi msomaji wa blog hii ya  tanga kunani kumbuka haya ni mauzauza ambayo Bwana Musa Hamadi mtumishi wa chumba cha maiti kataka hospitali ya Bombo alikutana nayo,lakini istoshe mara baada ya wiki moja kupita mara baada ya tukio hilo hapo juu lilitokea tukio jengine  majira ya saa nne asubuhi akiwa amekaa ofisi kwake aliona wanawake watatu,wawili wakiwa wamevaa baibui na mmoja alikuwa amevaa kanga  wakiwa chini ya mwembe  ambapo  palikuwa pana wagonjwa  wakipika chai basi wanawake hawa walisimama sana ndipo walipoelekea mochwari upande ule wa kutolea maiti ndipo  Bwana hamadi akahisi wale wanawake wamekwenda kule nyuma kujisaidia ambapo hawaruhusiwi watu kujisaidia na alipofika  hakuwakuta kabisa na alitafuta kama mara tatu hadi nne bila mafanikio yoyote alijiuliza kuwa ni vioja gani tena hivi.

Hata hivyo kundi la pili la mauzauza ya Bwana Hamadi katika chumba cha maiti ambayo hatokaa kuyasahau ni yale ya kubadilishiwa maiti,ambapo siku moja katika chumba cha maiti palikuwa na maiti wawili tu mmoja alikuwa mwanammke na mmoja alikuwa ni mwanaume,huyu mwanaume alioshwa na kuvishwa sanda tayari huku akiwa yupo katika chumba cha kuoshea maiti na baadae wakaja watu wakataka maiti yao wakaizike ndipo Bwana Hamadi akawaleza kuwa maiti yenu ipo katika chumba cha kuoshea maiti wale wakakataa kabisa kuwa hapana sisi maiti yetu tulimwacha hapa sasa yule sio wetu  basi sisi twamchukua huyu hapa wakajibiwa kuwa hapana huyu sio wenu na huyu hapa  ni mwanammke ambae ni mtumishi wa manispaa sasa kama mna uhakika chukueni lakini huyu ni mwnamke,ndipo wakaondoka na Yule maiti ambae si yao hadi maeneo ya Kwale mkinga kwa ajili ya mazishi na wakafanikiwa kumzika.

Siku inayofata yaani siku ya pili mwenye maiti yake akiwa amefika na kibali kwa ajili ya kuchukua maiti yake kwenda Lushoto kwa ajili ya mazishi,kuangalia wakakuta maiti ni mwanamme ndipo wakasema kuwa hapana huyu si maiti yetu sisi maiti yetu ni mwanamke na namtaka maiti yangu mwanammke.
Kilichofata hapo ni kuchukua gari kwenda Kwale kuchukua maiti ile iliyozikwa tayari na kuwapelea maiti ya kwao ambayo ndio ile ilokuwepo pale chumba cha maiti,walipofika walikuta viongozi wakawaleza na kuwaonesha maiti yao walipoiona tu kweli walithibitisha ndio yakwao kwani yule walifanya makosa kuichkua.Ndipo taratibu sasa za kwenda kuifukua maiti zikaanza,na Bwana Hamadi na wenzake walipoelekea hadi makaburini na kwenda kumfukua maiti yule wakaichukua wakarudi nayo wakaisafisha na kuipiga dawa  ikawa safi kabisa na kuwakabidhi wenyewe maiti yao.

Ukiachana na mauzauza aliyokutana nayo mtumishi huyo wa chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Bombo Tanga pia aliwahi kukutana na  maiti za ajali amabazo kwake hizo ndio nyingi mno  huku kupokea maiti za ajali zilizoua na kwa mara ya kwanza kuwahi kupokea maiti zaajali ni  ile ajali iliyoua watu si chini ya 35  watu walioanguka na kijigari  kilichokua kikitokea Duga maforoni  kikangukia  maeneo ya mzambarauni .Hata hivyo anazikumbuka ajali zilizoua watu wengi pia kama ile ya No  Challenge iliyoua watu takribani 46 na ile ya magogo  na basi iliyoua watu takribani hamsini ama Sitini.

Kuna taarifa za mitaani kuwa watu wakienda kuchukua maiti zao hua wanatolewa maiti ambazo si zao na huwa zimeharibika aidha zilizopta ajali na zinatisha ili utoe pesa kidogo  uoneshwe maiti yako,kumbe taarifa hizi si za kweli na Bwana Hamadi ameziita taarifa hizi kuwa ni maneno ya kwenye kahawa kwani hapendi kuharibu kazi yake aidha kwa kulewa ama kuomba pesa ambapo kwa mujibu kazi yake ni kosa na linaweza kusababisha pia kupoteza kazi yake labda mtu apende mwenyewe kumpa chochote. Tembelea Hapa Kusikiliza Mauza uza haya



1 comment: