Mauza
uza ya hospitali ya Bombo
Na Kassim Discover
Msomaji wa Blog hii ya tanga Kunani wakati
naianza safari yangu ya kuianda makala hii ilikuwa ni muda wa usiku ndipo kila nikizidi
kwendambele zaidi nahisi kama woga flani hivi
kwa jinsi mauza uza haya yalivyomtokea msimamizi wa chumba cha maiti
hospitali ya Bombo huku nikijiuliza swali je,kama mimi au wewe unatokewa na hali kama hizi dahhhhhhhhhh weeeeeeeeeee lazima kivumbi kingetokea na mengi yangesemwa tu!
Jengo la chumba cha kuhifadhia Maiti katika Hospitali ya Bombo |
Musa Hamadi ni mtumishi
katika Hospitali ya Bombo Tanga
chumba cha kuhifadhia maiti
yaaani mochwari,Bwana Musa Hamadi aliianza kazi katika chumba cha maiti mnamo tarehe
8/9/1981 hadi wakati huu licha ya kukutana na changamoto na mauza uza
mbali mbali katika kazi hiyo ambayo yamempa ujasiri wa hali ya juu na kuzidi
kuizoea kazi yake hiyo, kazi yake kubwa
hapo ni kuhifadhi maiti ambazo zimetoka wodini ama nyumbani kwa heshima
zote kwa kuiweka sehemu nzuri katika jokofu zake za kuhifadhia maiti hiyo mpaka pale ndugu wa marehemu watakapofatilia maiti yao kwa ajili ya mazishi
ndipo huwakabidhi wahusika.
Kwa wale wanaofatilia maiti zao huwa wakifika
mochwari humtajia jina la maiti huyo ambapo yeye kama muhusika kwa uzoefu wake
huwa anaingia katika chumba cha maiti na
kuwatolea ama kuwaonesha wahusika maiti zao ambazo huifadhiwa katika majokofu
huku kila jokofu likiwa na jina la marehemu na huku wakitakiwa wawe na kibali
kutoka katika wodi aliyofika marehemu yaani ‘’Death Certificate’’.
Bwana Hamadi
ni hodari sana katika kuzifanyia
uchunguzi maiti ambazo bado hazijafanyiwa ucgunguzi aidha zilizopelekwa hapo na
jeshi la polisi ambazo bado hazijafanyiwa,ambapo ujuzi na utaalamu huo ameupata
hapo hapo hospitali ya Bombo na kule mjini Morogoro alikokwenda katika semina
ya uchunguzi, zaidi akimshukuru marehemu Dokta Muhina aliekuwa Daktari katika
hospitali hiyo kwa kumfundisha kazi hii
ya uchunguzi yaani ‘’Prosmoter Investigation’’.
Kama nilivyokwambia hapo awali mpenzi msomaji
wa Tanga Kunani kuwa wakati naiandaa
makala hii hali flani ilinijia kama hofu flani hivi kutokana na kusisimua kwake
na sasa hebu nifatilie kwa makini sasa ufahamu mauzaza hayo ya ya Mochwari.
Kuna mauzauza ya
aina mbili ambayo msimamizi au mtumishi wa mochwari Ndugu Musa Hamadi aliwahi
kukutana nayo miaka hiyo ya nyuma ni kuwa mnamo mwaka 1988 mida ya saa saba za
mchana akiwa ofisi kwake amejipumzisha
alisikia ghafla mlango ukifunguliwa kwa kasi ya ajabu huku watu wakitembea huku zikitoka sauti kama za mtu au watu waliovaa
viatu vya kokoko,alishangaa sana akajiuliza ni nani walioingia humu ndani bila
ya mimi kuwaruhusu au ni kina nani wanaoosha maiti bila ruhusa yangu? Akajipa
moyo zaidi ikamlazimu afatilie ndani ili
awajue ni kina nani hao walioingia bila taarifa lakini cha kushangaza hadi alipofika
mlangoni alikuta mlango umefungwa kama ulivyo na hakukuwa na ishara yoyote ile
ya mlango kama umefunguliwa ama kufungwa,alishangaa sana kuona hivi akarudi zake kupumzika lakini mara
baada ya muda mchache kupita hivi akasikia
upepo mkali unavuma ndani,akaingia tena hadi ndani hakukuta mtu wala
kitu chochoe kile lakini alijipa moyo zaidi kwa kuwa wapo karibu na bahari
labda ni mambo ya majini jinni tu huku mwenyewe hakikataa kuamiani kama kweli yapo.Licha ya Ndugu Hamadi kukutana
na mauzauza mengi siku nyengine alikuwa akiwa amekaa ikaja pickup nyeupe ikiwa
na watu kama sita hivi akiwemo dereva pamoja na watu wengine waliomo yaani kama
vile wanakuja kuchukua maiti walikuja wakaelekea moja kwa moja hadi upande wa
nyuima wa mochwari,ndipo Bwana Hamadi ikabidi
awafate labda inaweza ikawa hawa watu ni
wageni hawaelewi mlango wa kwenda kuchukulia
maiti ni upi lakini pia cha kushangaza na cha ajabu alizunguka mochwari kama mara mbili hakuona
gari wala mtu yoyote wala dalili ya mtu kwenda huku akijiuliza bila kupata
majibu asijue ni wapi walipokwenda watu wale walokuja.
Mpenzi msomaji
wa blog hii ya tanga kunani kumbuka haya
ni mauzauza ambayo Bwana Musa Hamadi mtumishi wa chumba cha maiti kataka
hospitali ya Bombo alikutana nayo,lakini istoshe mara baada ya wiki moja kupita
mara baada ya tukio hilo hapo juu lilitokea tukio jengine majira ya saa nne asubuhi akiwa amekaa ofisi
kwake aliona wanawake watatu,wawili wakiwa wamevaa baibui na mmoja alikuwa
amevaa kanga wakiwa chini ya mwembe ambapo
palikuwa pana wagonjwa wakipika
chai basi wanawake hawa walisimama sana ndipo walipoelekea mochwari upande ule
wa kutolea maiti ndipo Bwana hamadi
akahisi wale wanawake wamekwenda kule nyuma kujisaidia ambapo hawaruhusiwi watu
kujisaidia na alipofika hakuwakuta
kabisa na alitafuta kama mara tatu hadi nne bila mafanikio yoyote alijiuliza
kuwa ni vioja gani tena hivi.
Hata hivyo kundi
la pili la mauzauza ya Bwana Hamadi katika chumba cha maiti ambayo hatokaa
kuyasahau ni yale ya kubadilishiwa maiti,ambapo siku moja katika chumba cha
maiti palikuwa na maiti wawili tu mmoja alikuwa mwanammke na mmoja alikuwa ni mwanaume,huyu
mwanaume alioshwa na kuvishwa sanda tayari huku akiwa yupo katika chumba cha kuoshea
maiti na baadae wakaja watu wakataka maiti yao wakaizike ndipo Bwana Hamadi
akawaleza kuwa maiti yenu ipo katika chumba cha kuoshea maiti wale wakakataa
kabisa kuwa hapana sisi maiti yetu tulimwacha hapa sasa yule sio wetu basi sisi twamchukua huyu hapa wakajibiwa kuwa
hapana huyu sio wenu na huyu hapa ni mwanammke
ambae ni mtumishi wa manispaa sasa kama mna uhakika chukueni lakini huyu ni
mwnamke,ndipo wakaondoka na Yule maiti ambae si yao hadi maeneo ya Kwale mkinga
kwa ajili ya mazishi na wakafanikiwa kumzika.
Siku inayofata
yaani siku ya pili mwenye maiti yake akiwa amefika na kibali kwa ajili ya
kuchukua maiti yake kwenda Lushoto kwa ajili ya mazishi,kuangalia wakakuta
maiti ni mwanamme ndipo wakasema kuwa hapana huyu si maiti yetu sisi maiti yetu
ni mwanamke na namtaka maiti yangu mwanammke.
Kilichofata hapo
ni kuchukua gari kwenda Kwale kuchukua maiti ile iliyozikwa tayari na kuwapelea
maiti ya kwao ambayo ndio ile ilokuwepo pale chumba cha maiti,walipofika
walikuta viongozi wakawaleza na kuwaonesha maiti yao walipoiona tu kweli
walithibitisha ndio yakwao kwani yule walifanya makosa kuichkua.Ndipo taratibu
sasa za kwenda kuifukua maiti zikaanza,na Bwana Hamadi na wenzake walipoelekea
hadi makaburini na kwenda kumfukua maiti yule wakaichukua wakarudi nayo
wakaisafisha na kuipiga dawa ikawa safi
kabisa na kuwakabidhi wenyewe maiti yao.
Ukiachana na
mauzauza aliyokutana nayo mtumishi huyo wa chumba cha kuhifadhia maiti katika
hospitali ya Bombo Tanga pia aliwahi kukutana na maiti za ajali amabazo kwake hizo ndio nyingi
mno huku kupokea maiti za ajali zilizoua
na kwa mara ya kwanza kuwahi kupokea maiti zaajali ni ile ajali iliyoua watu si chini ya 35 watu walioanguka na kijigari kilichokua kikitokea Duga maforoni kikangukia
maeneo ya mzambarauni .Hata hivyo anazikumbuka ajali zilizoua watu wengi
pia kama ile ya No Challenge iliyoua watu
takribani 46 na ile ya magogo na basi
iliyoua watu takribani hamsini ama Sitini.
Kuna taarifa za
mitaani kuwa watu wakienda kuchukua maiti zao hua wanatolewa maiti ambazo si
zao na huwa zimeharibika aidha zilizopta ajali na zinatisha ili utoe pesa kidogo uoneshwe maiti yako,kumbe taarifa hizi si za
kweli na Bwana Hamadi ameziita taarifa hizi kuwa ni maneno ya kwenye kahawa
kwani hapendi kuharibu kazi yake aidha kwa kulewa ama kuomba pesa ambapo kwa
mujibu kazi yake ni kosa na linaweza kusababisha pia kupoteza kazi yake labda
mtu apende mwenyewe kumpa chochote. Tembelea Hapa Kusikiliza Mauza uza haya
Duhhhhh si utani
ReplyDelete