Kundi la wapiganaji wa kisomali Al-shabaab
limethibitisha kuwa kiongozi wake Ahmed Abdi Godane aliuawa siku ya
jumatatu katika shambulizi la angani lililotekelezwa na wanajeshi wa
Marekani.
Msemaji wa Alshabaab amesema kuwa wanachama
wengine wawili wa kundi hilo pia walifariki katika shambulizi hilo
,yapata kilomita 170 kusini mwa mji mkuu wa Mogadishu .
Ripoti zinasema kuwa kundi la Alshabaab
limemchagua kiongozi mpya Ahmad Omar,katika mkutano uliofanyika katika
eneo lisilojulikana.
Chanzo BBC

No comments:
Post a Comment