MSHAMBULIAJI mpya wa Arsenal, Danny Welbeck jana alikuwa ana
nafasi nzuri ya kuwa shujaa wa timu hiyo katika mchezo wa kwanza wa
hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borrusia Dortmund,
lakini akashindwa kuitumia.
Mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 16 kutoka kwa wapinzani, Manchester United jana alienedelea kupewa nafasi katika kikosi cha kwanza cha The Gunners na kocha Arsene Wenger akionyesha alimsajili kwa sababu alimuamini, lakini akashindwa kuwafurahisha mashabiki.

![]() | ||||
Haamini macho yake; Mshambuliaji mpya wa Arsenal, Danny Welbeck akiwa amepiga magoti kwa masikitiko baada ya kupoteza nafasi nzuri ya kufunga kipindi cha kwanza jana |
Muingereza huyo jana alipata nafasi tatu nzuri za kuifungia
Arsenal mabao kuanzia mapema kipindi cha kwanza, lakini zote akashindwa
kuzitumia, The Gunners wakichapwa mabao 2-0 na Dortmund ugenini.
Dhahiri Welbeck anahitaji kujiuliza mno baada ya mechi ya jana, kwani iwapo atarudia makosa aliyoyafanya katika mchezo huo, atajitengenezea mazingira ya kuondoka kwenye kikosi cha kwanza Gunners.
Dhahiri Welbeck anahitaji kujiuliza mno baada ya mechi ya jana, kwani iwapo atarudia makosa aliyoyafanya katika mchezo huo, atajitengenezea mazingira ya kuondoka kwenye kikosi cha kwanza Gunners.
![]() |
Mshambuliaji wa Arsenal, Danny Welbeck alipata nafasi nzuri ya kufunga hapa bao ambalo lingekuwa la kuongoza kwa Arsenal, lakini akakosa mpira ukimpita namna hii. |
![]() |
Nyingine hii; Danny Welbeck akianguka chini na kumshuhudia kipa wa Dortmund, Roman Weidenfeller akienda upande mwingine wa lango na mpira ukitoka nje baada ya kushindwa kuunganishia nyavuni |
Na hii tena; Welbeck akapata nafasi nyingine tena, lakini akapiga juu ya lango | Source: Bin Zubeiry |
No comments:
Post a Comment