Home Traders

Home Traders

Tembelea TK FM Redio 88.5 Tanga

Thursday, 18 September 2014

Said Konomi kuzikwa Kesho!!!

Hakuna asiemfahamu Said Konomi hapa Tanga kwa staili yoyote ile labda tu kama hujabahatika kuishi hapa Tanga au umekuja ukiwa mtu mzima.
Huyu ni mtu ambaye alikuwa akifahamika zaidi katika msikiti wa Anisa uliopo barabara ya kumi na Saba.
KONOMI alikuwa  akikuhubiria kuhusu mauti au kumuabudu mola wako na kuuvaa uhusika mpaka unaogopa na kutetemeka mwenyewe uwapo kitandani.
Hatimae leo hii amefariki dunia kama masaa manne yaliyopita na anatarajiwa kuzikwa hapo kesho majira ya saa nne.
Hizo ndizo taarifa zilivyonifikiwa kuhusu mazishi yake siku ya kesho,haya sasa wana Tanha shime shime tujitokezeni kumsindikiza mzee wetu.
Kama kuna chochote wana Tanga basi tupeane taarifa kupitia hapa hapa.
Mungu ailaza roho ya marehemu Said Konomi mahala pema peponi Amiin.
Comment toka Facebook kwa Abdalah Sady

No comments:

Post a Comment