Familia ya Reeva Steenkamp ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi na mwanariadha wa Afrika kusini Oscar
Pistorius imekasirishwa na uamuzi wa jaji wa kesi hiyo baada ya kumpata
na hatia ya mauaji ya kutokusudia na kumuondoalea mashtaka ya mauaji.
![]() |
Familia ya Marehemu Reeva Steenkamp |
June Steenkamp amesema kuwa mwanawe ambaye alikufa vibaya hakufanyiwa haki.
Amesema
kuwa hakuamini kwamba jaji wa kesi hiyo alikubali ushahidi wa Oscar
Pistorius kwamba alidhani bi Reeva Steenkamp alikuwa mtu ambaye alikuwa
amevamia nyumba yao.
Hatahivyo mjombaake Pistorius alimshukuru jaji huyo kwa kumuondolea mashtaka ya mauaji mwanariadha huyo.
Oscar Pistorius ataendelea kuwa nje kwa dhamana hadi hukumu yake itakapotolewa mnamo mwezi ujao.
Chanzo BBC
Chanzo BBC
No comments:
Post a Comment