Waziri wa maswala ya
kigeni nchini Marekani John Kerry amepinga ripoti kwamba mataifa ya
kiarabu hayaungi mkono moja kwa moja juhudi zake za kubuni muungano wa
kukabiliana na kundi la wapiganaji wa himaya ya kiislamu.
![]() |
John Kerry nchini Uturuki |
Akizungumza nchini Uturuki katika ziara ya eneo la mashariki ya kati,amesema kuwa ameridhishwa na majibu aliyopata kutoka Saudi Arabia na mataifa mengine.
Lakini amesema kuwa si sahihi kwa Iran kujiunga na juhudi za kimataifa dhidi ya wapiganaji hao.
Bwana Kerry anatarajiwa kuelekea nchini Misri hii leo.
Mataifa kumi ya kiarabu yamekubali kuisaidia marekakani.
Chanzo BBC
No comments:
Post a Comment