Home Traders

Home Traders

Tembelea TK FM Redio 88.5 Tanga

Monday, 8 September 2014

Sarafu ya 500 Kuanza rasmi mzunguko Oktoba

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imezindua rasmi sarafu mpya ya Sh500 itakayoanza kuingia katika mzunguko wake  Oktoba mwaka huu.
Muonelano wa Sarafu mpya
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa huduma za kibenki wa BoT, Emmanuel Boaz alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Daressalaam na kusema kuwa  Serikali imefanya uamuzi huo ili kurahisisha upatikanaji wa chenji na kutunza ubora wa fedha.
“Noti ya Sh500 ndiyo inayopitia mikononi mwa wananchi wengi hivyo kuchakaa mapema. Lakini kutokana na gharama ya kuzichapisha ukilinganisha na sarafu ambazo hudumu kwa muda mrefu, tumeamua kuziondoa noti na kuleta sarafu yenye thamani ile ile.
Aliendelea kusema kua Kuna taratibu zinaendelea kukamilishwa kabla hazijaingizwa katika mzunguko mnamo mwezi wa kumi mwaka huu.
Aidha Bwana Emmanuel ameendelea kusema kua  sarafu hizo  zitakapoanza kutumika hakutakuwa na haja ya wananchi kwenda kubadilisha noti walizonazo kwani zitakuwa zinatumika pamoja hadi zitakapopotea katika mzunguko.
Sarafu hiyo ina umbo la duara, lenye kipenyo cha milimita 27.5 na michirizi pembeni ikiwa na uzito wa gramu 9.5. Mbele ina picha ya Rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Aman Karume na nyuma ni nyati.
Pesa hiyo ya Shillingi Mia Tano iliwahi kupitia katika hatua mbali mbali tazama hapo chini kama zinavyoonekana ya picha zake.

No comments:

Post a Comment