Baadhi ya vituo vya Redio vilivyopo hapa jijini Tanga kikiwemo BREEZE FM na vile vya mkoa wa Morogoro vitabadilishiwa masafa na kupewa mengine mapya hivi karibuni.
Kwa mujibu wa Muhandisi wa
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Ndugu Andrew Kisaka amesema hayo
leo hii asubuhi wakati akizungumza na shirika la habari la utangazaji
TBC iliyopo jijini Daresalaam kuwa vituo hivyo vinabadilishiwa masafa hayo kutokana na kuongezeka kwa vituo vya Redio mkoani Tanga na kuingiliana kwa masafa kwa baadhi ya Redio.
Hata hivyo Inginia Kisaka wakati akijibu swali la kwanini vituo hivyo vya Redio vinaingiliana masafa,alisema kuwa hii inatokana na kutokuwepo sehemu moja kwa minara ya kurushia matangazo ambapo hivi ndio inatokana kuingiliana kwa masafa hayo.
Hata hivyo Inginia Kisaka amesema kua suluhisho pekee la kutatua tatizo hili la kuingiliana kwa masafa ni kuwaagiza sasa vituo vyote vya Redio kununua kifaa kinachojulikana kama (FILTA) ambacho hiki kitakuwa kikichuja mwenendo mzima wa masafa na kuzuia mwingiliano.
Ikumbukwe kua kubadilishwa kwa masafa hayo ni mwendelezo wa mamlaka hayo ambapo ikumbukwe kua zoezi hili pia liliwahi kufanyika pia katika jiji la Daressalaam na sasa ni zamu ya jiji la Tanga na mkoa wa Morogoro.
No comments:
Post a Comment