Kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom
Tanzania imezindua huduma mpya ya M-PESA inayojulikana kama"LIPA KWA
M-PESA huduma hii mpya ni sambambsa kabisa na mfumo wa malipo utakao
wezesha makampuni,mawakala wa jumla na rejareja na wafanyabiashara
wengine kulipia bidhaa zao kwa kutumia M-PESA.
![]() |
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Kelvin Twissa (katikati) akiongea na waandishi wa |
Huduma
hii mpya imekuja ili kuboresha mazingira ya wafanyabiashara na
makampuni kwa kupanua mbinu za malipo kutoka kwa wafanyabiashara na
makampuni na wauzaji wa aina mbalimbali, sasa mawakala wa jumla na
rejareja wataweza kununua na kulipia bidhaaa zao kwa kutumia huduma hii
ya LIPA KWA M-PESA. Njia hii mpya ni ya haraka, salama na inampa mteja
wepesi zaidi wa kufanya biashara.
No comments:
Post a Comment