
Kutokana na hali hiyo, wanachama hao wakiongozwa na James Haule,
wamemuandikia Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi,
kuelezea kusikitishwa kwao na ofisi yake kukaa kimya juu ya hali hiyo.
Katika barua yao kwenda kwa msajili isiyokuwa na namba ya kumbukumbu
ya Septemba 15 mwaka huu, wanachama hao wameeleza kuwa uchaguzi wa TLP
ulipaswa kufanyika Januari 31 mwaka huu na kwamba, kuanzia siku hiyo
mwenyekiti wao alipoteza sifa ya kuwa kiongozi.
Ilieleza, Wanachama wa TLP wanayo heshima kubwa ya kuandika barua
hiyo kwa matumaini ya kupata ufumbuzi wa ukiukwaji wa katiba ya chama
chao, ikiwa ni pamoja na sheria za nchi zinazowaongoza katika kufanya
uchaguzi wa kidemokrasia.
“Kutokana na kukiukwa kwa katiba… sisi wanachama tunaitaka ofisi yako
kutoa mwongozo juu ya uitishwaji wa mkutano mkuu wa Chama kuanzia ngazi
ya matawi hadi Taifa, kwa kuwa Chama sasa hakina viongozi, kwani
waliopo sasa wamekosa sifa kuanzia Januari 31 mwaka huu,” ilisema barua
hiyo.
Kwa upande wake, Mrema ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo, alipulizwa juu
ya ukiukwaji wa katiba ya chama chake na kwamba hawako madarakani kwa
mujibu wa katiba yao, alisema hawezi kujiongezea muda wa kuongoza bila
kuungwa mkono na Katiba iliyopo.
Alisema anachojua kufanya jambo lolote kinyume na taratibu za kisheria ni kosa na kwamba, hawezi kuingia katika mtego huo.
“Mimi si mwendawazimu, nataka nikwambie misingi na kanuni iliyoniweka
madarakani mpaka muda huu, lakini kwanza nipe dakika tano niwasiliane
na wenzangu,” alisema Mrema.
Hata hivyo, baada ya kupigiwa simu katika muda aliyotoa, bado hakuwa
na jibu la uhakika juu ya kipengele kinachompa fursa ya kuendelea kuwa
madarakani huku akimtaka mwandishi aendelee kuvuta subira.
Hatua ya wanachama wa TLP kumkataa Mwenyekiti wao, ni muendelezo wa
misukosuko inayompata kiongozi huyo katika uwanja wa siasa, baada ya
hivi karibuni kukaririwa akimuomba Rais Kikwete amuondoe James Mbatia
katika nafasi ya Ubunge ili asiweze kumpokonya Jimbo la Vunjo.
Chanzo Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment