Wanajeshi kutoka nchini Libya
wamerejeshwa nchini kwao kutokana na kukosa uadilifu wakiwa mafunzoni
Uingereza huku wengine wakituhumiwa kufanya vitendo vya ukatili wa
kimapenzi.
Wanajeshi hao waliokuwa mafunzoni nchini Uingereza, 300
kati yao wamesharejeshwa Libya kutokana na tuhuma kuhusiana na
unyanyasaji wa kimapenzi.
![]() |
Wanajeshi wa Libya |
Waziri wa Ulinzi wa Libya amethibitisha kurejeshwa kwa askari hao na kuongeza kuwa wengine watarejeshwa siku chache zijazo.
wanajeshi
wawili wa Libya wamekiri kufanya vitendo vya unyanyasaji wa kingono
dhidi ya wanawake huko Cambridge, ambapo wawili wameshafikishwa
mahakamani wakikabiliwa na mashitaka ya ubakaji.
Baadhi ya wakazi
wa eneo jirani na kambi ya jeshi walipo wanajeshi hao wa Libya,wamesema
kuwa wamekuwa wakiwaona wanatoka nje ya ngome za jeshi kwaajili ya
kununua pombe, na tayari waziri wa ulinzi amekiri kupokea mashtaka hayo
na kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya wanajeshi hao wa kigeni.
Waziri
Libya amesema wanajeshi hao wanaruhusiwa kutoka nje ya kambi kwa saa
tatu wiki kwani ameongeza kuwa madhara ya askari hao kuzagaa mitaani ni
makubwa na wengine hujitumbukiza katika matumizi dawa za kulevya na
ulevu wa kupindukia.
No comments:
Post a Comment