Vyama vya siasa nchini Burkina Faso
vimekubaliana kuwa na uchaguzi mkuu mwezi Novemba 2015 ikiwa ni harakati
za kurejesha utawala wa kiraia na demokrasia..
![]() |
Luten Kanal Isaac Zida |
Hata hivyo
mazungumzo hayo yameisha bila kuwa na ufumbuzi kuhusiana na nani
atakayekuwa kiongozi wa mpito hadi kufikia muda wa kufanyika kwa
uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kufuatia kuangushwa kwa aliyekuwa raisi wa
taifa hilo la Afrika Magharibi Blaise Compaore.
Jeshi la nchi hiyo
limekuwa likishikilia madaraka ya tangu aondolewe madarakani kutokana
na maandamano ya raia waliokuwa wakishinikiza Rais Compaore.
Umoja
wa Afrika jumatatu wiki hii umetoa muda wa wiki moja kufanyika kwa
mabadiliko ya utawala na kukabidhiwa kwa wananchi na siyo jeshi tena.
Luten
Kanal Isaac Zida ambaye ni kiongozi wa mpito wa kijeshi ameahidi
kufuata ushauri huo wa umoja wa Afrika kwa kukabidhi madaraka kwa
wananchi ndani ya muda huo wa wiki mbili.
No comments:
Post a Comment