Katika harakati za kusaka nafasi ya kutaka
kuteuliwa na chama chake kwa ajili ya
kupewa ridhaa ya kugombea urasi na kuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania
Mheshimiwa waziri Mkuu Mizengo kayanza Peter
Pinda hatimae siku ya leo alikuwepo hapa Tanga mchana katika ofisi za ccm mkoa na kujipatia jumla ya wadhamini 1435
waliojitokeza kumdhamini.
 |
Picha na Miktaba |
Pinda akizungumza na wanachama wa chama hicho
katika ofisi za chama hicho zilizopo Barabara ya 21 amesema kuwa
katika watu 41 waliojitokeza kuomba ridhaa katika chama chao,amesema kuwa mgombea yoyote
atakaechaguliwa atamuunga mkono huku akiwaomba pia wanachama wa chama
hicho wamuunge mkono atakaechaguliwa na ambao
pia hawatabahatika kuchaguliwa wasinung’unike.
Pia amempongeza Mbunge viti maalum wa ccm Ummy Mwalimu kuwa
ni jembe linalofanya kazi yake kisawa sawa huku akiwaasa wanawake kuwa wamtumie
vizuri basi wanaweza kufika mbali zaidi.
Na hata hivyo amewashukuru sana wana Tanga
kwa mapokezi yao kwake.
No comments:
Post a Comment