Home Traders

Home Traders

Tembelea TK FM Redio 88.5 Tanga

Saturday, 30 July 2016

Azm fc kuwasili jijini Daressalaam kesho kutokea Zanzibar



Timu ya Azam fc kesho inatarajiwa kuondoka kisiwan Zanzibar  ilipokuwa imeweka kambi kwa siku kadhaa kurejea  jijini Daressalam  mara baada ya kumalizia mchezo wao wa kirafiki watakaoucheza leo na timu ya taifa ya Jangombe  usiku wa Saa mbili na nusu.
Jafary Idd
 Akizungumza na TK FM REDO mkurugenzi wa habari na mawasiliano watimu hiyo Jafary Idd Maganga amesema kuwa mara baada ya mchezo wa leo kesho saa tatu asubuhi timu inatarajiwa kuondoka  kisiwani kurejea jijini Daressalam.
Aidha Maganga amesema kuwa wachezaji wawili Golikipa Mwadini Ally Na Ame Ally Zungu wamekwenda Simba Sports Club kwa mkopo na golikipa Aishi Manula kama watu wanavyodai.
Maganga amefafanua kuwa Simba wameleta barua za kuwaomba wachezaji hao wawili na ndipo  wachezaji hao kukaa na uongozi ndipo walipokubali kwenda Simba kwa makopo.

No comments:

Post a Comment