Home Traders

Home Traders

Tembelea TK FM Redio 88.5 Tanga

Saturday, 30 July 2016

Muda mchache baada ya kutangazwa miss Tanga,Eligiva Mwasha Afunguka kwa wana Tanga

Mshindi wa taji la Miss Tanga 2016 Eligiva Mwasha amewashukuru wana Tanga  kwa ujumla kwa sapoti yao waliomuonyesha jana katika  fainali za miss tanga 2016 hivyo kuwataka wanatanga kumuombea kwani kwa sasa  safari aliokua nayo bado kubwa sana kwani anamtihani wakwenda kuiwakilisha Tanga katika fainali za Miss Kanda  na badae kulekea Katika fainali za miss Tanzania baadae mwaka huu.
Mshindi wa taji la TK FM MISS TANGA 2016 Elgiva Mwasha akiwa katika pozi la kawaida
 Hata Hivyo Eligiva ameishukuru sana  familiya ndugu jama na marafiki waloonyesha ushirikiano wao na kuahidi kufanya vizuri katika mashindano ya kanda na Tanzania kiujumla.
Eligiva ni mshindi wa taji la miss Tanga alilolitwaa jana  tarehe 29/7/2016 katika hoteli ya Tanga Beach Resort & Spa baada ya kuwashinda wenzake tisa.
Tano Bora ya Miss Tanga kama inavyoonekana katika picha ya pamoja ambayo ndio iliyotoa mshindi wa Miss Tanga Jana kushoto namba 10 Asha Ally,Beatrice Mwangili,Edina Kisabo,Rukaiya Hassan na mshindi Eligiva Mwasha

Mshindi wa pili katika fainali hizo alikuwa ni Asha Ally na mshindi wa tatu alikuwa ni  Rukaiya Hassan.

Fainli za Miss Tanga mwaka huu zinajulikana kama TK FM MISS TANGA 2016 zimeandaliwa na kituo maarufu cha redo jijini Tanga 88.5 TK FM REDIO wakishirikiana na Tanga Beach Resort.


No comments:

Post a Comment