Kutokana
na maombi ya klabu nyingi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kutaka kuandaa
wachezaji wake kwa ajili ya Ligi Kuu msimu unaoanza sasa, umemlazimu Kocha Mkuu
timu hiyo Charles Boniface Mkwasa kuahirisha kambi iliyokuwa ianze Jumatatu
Agosti mosi, mwaka huu.
![]() |
Kocha Mkuu wa Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa |
Wachezaji
ambao Mkwasa amewaita wanatoka kwenye klabu mbalimbali na ambazo zinaongoza
kutoa nyota wengi ni Simba SC, Young Africans SC, Azam FC na Mtibwa Sugar FC.
Hivyo
basi kutokana na hivyo Mkwasa sasa
atakuwa anafuatilia mwenendo wa nyota 24 aliowaita kwenye michezo mbalimbali ya
kirafiki wa klabu hizo inayofanyika kabla ya kuanza Ligi Kuu Tanzania Bara
(Pre-season matches) na michezo ya raundi ya kwanza na pili ya Ligi Kuu kabla
ya kukiita tena kikosi hicho kwa ajili ya safari ya kwenda Nigeria.
Taifa
Stars ina mchezo na jijini Lagos, Nigeria Septemba 2, 2016 ambao ni wa
kukamilisha ratiba katika kundi G baada ya Misri kusonga mbele wakati Chad
kujitoa.
CHANZO TFF TANZANIA
No comments:
Post a Comment