Home Traders

Home Traders

Tembelea TK FM Redio 88.5 Tanga

Thursday, 28 July 2016

Tk fm Miss Talent 2016 watano wapenya fainali ZA TALENT sasa mshindi kutangazwa fainali Miss Tanga

Mashindano ya miss talent 2016 ambayo yamefanyika jana katika kiwanja cha kijanja cha tanga city lounge imeshuhudiwa warembo watano wakipenya tano bora ya miss talent ambapo mshindi wake atatangazwa siku ya fainali za miss tanga zinazotarajiwa kufanyika katika hoteli ya kitalii ya tanga beach resort & spa siku ya  ijumaa tarehe 29 mwaka huu.


Washiriki wa TK FM MISS TANGA 2016 wakia katika pozi tofauti kama wanavyoonekana  katika picha ya pmoja


Washiriki saba waliokuwa wakishindana  katika fainali hizo  ambao ni Felister George,Fatuma Makota,Glory Maimu,Aisha Ally, Rose Simon,Beatrice Mwangili pamoja na Edna Kisabo huku washiriki  wakiweza kuonyesha talent zao za kisasa kama urembo na mitindo,kucheza pamoja na ubunifu mbali mbali.

Chini ya majaji watatu waliokuwa makini usiku wa jana wakiongozwa na  jaji mkuu Tabu Raina akisaidinana na John Kingodi pamoja na Frank Kibaja waliweza kupata tano bora  ambayo itatoa mshindi wa miss Talent 2016 atakaevishwa taji usiku wa fainali za Miss Tanga.

Washiriki waliopenya tano bora usiku wa jana ni  Fatuma Makota, Glory Maimu, Aisha Ally,Rose Simon na Edna Kisabo.
Moja ya Mshiriki wa Miss Talent ambae amepenya tano bor akionyesha kipj chake hapo jan.

Fainali za TK FM MISS TANGA 2016 zitashereheshwa na wasanii mbali mbali wa Tanga kama Wazenji Classic Band pamoja na  vikundi vya DANCERS vya TANGA bila kusahau  kundi bora mwaka huu la NAVY KENZO wakiburudisha ipasavyo huku washiriki  kumi na moja wakishiriki fainali hizo.

Kiingilio katika siku hiyo ni shilling 10,000/= VIP 30,000/= Single na Couple 50,000/=


No comments:

Post a Comment