Rais wa Simba Evans Aveva akizungumza na waandishi wa habari leo |
Hata hivyo Uongozi
wa hiyo umepanga maadhimisho hayo kuzinduliwa
na mkutano mkuu wa wanachama utakaofanyika katika bwalo la maofisa wa Polisi
Oysterbay Jumapili Julai 31.
Akuzungumza na waandishi wa habari leo Rais
wa Simba, Evans Aveva amesema kuwa watawashangaza
mashabiki wao kwa ‘suprise’ kubwa ya wachezaji waliowasajili msimu huu kwani kuna
wachezaji ambao watatangazwa na kuwashangaza mashabiki wetu.
Kikosi
hicho cha Inter Club kitapambana na Simba katika mchezo wa tamasha la Siku ya
Simba ambayo litafanyika Agosti 8, siku ambayo Simba itakua inatimiza miaka 80
tangu kuanzishwa kwake mwaka 1936.
Inter Club
inanolewa na kocha wa zamani wa
Simba, Zdravko Logarusic ambaye ameinoa Simba msimu wa 2014/15 kabla ya
kutupiwa virago baada ya kufungwa mabao 3-0 na Zesco United katika tamasha la
siku ya Simba.
Wakati
huo huo Viongozi na wanachama mbalimbali wa Simba watachangia damu katika
hospitali mbalimbali ikiwa ni kuungana na jamii.
No comments:
Post a Comment