MWANAFUNZI
wa kike anayesoma darasa la sita katika shule ya msingi Zumnati iliyopo Wilayani Korogwe Mkoani Tanga
amegeuka mlezi baada ya mama yake kumtoroka mara kadhaa na kumtelekezea wadogo
zake wawili huku mmoja kati yao akiwa ni
mlemavu wa viungo.
TK FM
imetembelea nyumbani kwa msichana anayeishi katika kata ya masugulu wilayani
humo anayefahamika kwa jina la HELENA
THOMAS na kuzungumza naye,
ambapo amesema kuwa mama yake huwa na tabia ya kuondoka zaidi ya wiki mbili kwa
kisingizio kuwa anatafuta pesa za chakula.
Aidha
FELISTA
ISSA ambaye ni mwalimu wa mwanafunzi huyo amesema kuwa kitendo
kinachofanywa na mama huyo kimemfanya Helena kutokuwa na maendeleo mazuri
darasani kutokana na majukumu aliyonayo na kuwataka wakinamama kutokwepa
majukumu ya familia.
Hata
hivyo TK FM imezungumza na mtendaji
kata MUSSA TWAHA ambaye
amekiri kuwafahamu watoto hao na kusema kuwa jitihada za kumsaka mama huyo aliyekosa huruma
zikiendelea kwa ajili ya kumfikisha
katika vyombo vya sheria.
No comments:
Post a Comment