Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu
za rambirambi Mwenyekiti wa Klabu ya Majimaji ya Songea, mkoani Ruvuma,
Humphrey Millanzi kutokana na kifo cha mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Kelvin
Haule kilichotokea jana Agosti 18, 2016 kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Ruvuma.
Rais
Malinzi amemuelezea Haule kuwa alikuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya
timku ya Majimaji ya Songea na Lipuli ya Iringa hivyo ameacha alama ya ucheshi,
kujituma na uwajibikaji katika kufanikisha kazi zake katika timu ambazo
alichezea.
Salamu
za rambirambi za Rais wa TFF Malinzi pia zimekwenda kwa familia ya marehemu,
ndugu, jamaa na marafiki na kuwataka kuwa na moyo wa subira wakati huu mgumu wa
msiba wa Kelvin Haule.
Mwenyezi
Mungu aipumzishe roho ya marehemu Kelvin Haule mahala pema peponi.
Bwana
alitoa, Bwana alitoa, jina la Bwana lihimidiwe.
No comments:
Post a Comment