Mchezo
huo utakaoanza saa 9.00 alasiri Jumapili Agosti 21, 2016 kwenye Uwanja wa Azam
ulioko Chamazi – Mbagala, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam utachezeshwa na
Mwamuzi Noiret Jim Bacari wa Comoro akisaidiwa na Mmadi Faissoil na Said Omar
Chebli wakati mezani atakuwa Ali Mohamed Adelaid huku Kamishna wa mchezo huo
atatoka Somalia ambaye anaitwa Amir Abdi Hassan.
Jumamosi
Agosti 6, 2016, Serengeti ilitoka sare ya 1-1 na Afrika Kusini katika mchezo
uliofanyika Uwanja wa Dobsonville ulioko Soweto, Mji ulioko Kusini – Magharibi
mwa jiji la Johannesburg, mabao yote yalipatikana kipindi cha pili yakiwa ni ya
penalti kwa kila upande. Afrika Kusini ndio walioanza kupata penalti katika
dakika 65 iliyofungwa na Luke Gareth kabla ya Ally Msengi kuisawazishia
Serengeti Boys katika dakika ya 70.
Penalti
ya Afrika Kusini ilitokana na mmoja wa mabeki wa Serengeti Boys kumfanyia
madhambi Linamandla Mchilizeli wa Amajimbos ndani ya eneo la hatari wakati ile
ya Serengeti Boys ilitoakana na beki Luke Donn wa Amajimbos kunawa mpira eneo
la hatari. Mwamuzi wa mchezo huo alikuwa, William Koto kutoka Lesotho.
No comments:
Post a Comment