Home Traders

Home Traders

Tembelea TK FM Redio 88.5 Tanga

Friday, 19 August 2016

LIGI KUU BARA KESHO NI KESHO,VITA YA MASAU BWIRE NA TOBIAS KIFARU IMEREJEA TENA

Je kweli Simba  watahitaji kutumia mbinu na akili kushinda  katika mchezo wa kesho?Tusubiri tuone……


Pazia la Ligi Kuu Bara msimu mpya wa 2016/2017 litafunguliwa  kesho Jumamosi Agosti 20, timu 14 zitakuwa katika viwanja tofauti kusaka ushindi katika mechi zao za kwanza za msimu, mechi zote zitakuwa na ushindani mkubwa kwani kila timu haitaki kubaki nyuma, kila mmoja anahitaji kuanza kwa ushindi.

Simba vs Ndanda

Licha ya maandalizi mazuri waliyokuwa nayo Simba haitakuwa rahisi kwao kupata ushindi dhidi ya Ndanda kama wanavyodhani, Wekundu wa Msimbazi wanatarajiwa kupata upinzani mkubwa siku hiyo kutoka kwa Ndanda, timu hiyo kutoka Mtwara ni moja ya klabu ngumu Ligi Kuu  na wanacheza kwa ushirikiano na kujituma muda wote dimbani, kwa hakika patachimbika.

Simba inataka kurejesha heshima yake, na Ndanda wanataka kudhihirisha kuwa si wa kudharauliwa.

Mtibwa vs Ruvu Shooting

Achana na vita vya uwanjani, vita kubwa ipo baina ya wasemaji wa klabu hizo, ambao ni marafiki wakubwa, Mtibwa Sugar ambayo msemaji wake ni Thobias Kifaru na Ruvu Shooting ambayo inawakilishwa na Masau Bwire, wasemaji hawa ndio wanafanya mechi hii kuwa na mvuto hasa kutokana na maneno yao ya kejeli nje ya uwanja.Msimu uliopita Kifaru alimmisi sana swahiba wake masau na sasa vita vinaendelea.



Stand utd v/s mbao  fc

Timu ya mbao inaingia uwanjani ikiwa  imependa ligi kuu msimu huu huku ikicheza na timu ambayo imekubwa sana na migogoro ya kiuongozi huku kila  timu inahitaji  kushinda katika mchezo wa kesho lakini wengi wakiipa nafasi timu ya stand utd kutokana na uzoefu wa ligi hiyo.

Majimaji v/s tanzani prisons

Huu ni mchezo mwngine pia tukiushuhuda kesho  pale maji maji watakapowakaribisha  Tanzania prisons huku timu zote zikiwa na uzoefu na mikiki mikiki ya ligi kuu Tanzania bara.

Azam fc v/s African Lyon

Mchezo huu utachezwa usiku pale chamanzi badala ya saa kumi  jioni kutokana na kesho jumaosi kutakuwa na mazoezi ya timu ya afrika kusini chini ya umri wa miaka 17 kuutumia uwanja wa chamanzi kwa ajili ya kufanya mazoezi.

HATA HIVYO

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaonya timu kuchezesha wachezaji wa kigeni kama hawana vibali vya kuishi, kufanya kazi na leseni inayomruhusu kucheza ligi husika kwa mujibu wa sheria za nchi na kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Vibali vya kuishi na kufanya kazi vinatolewa na Idara ya Uhamiaji Tanzania (Uhamiaji) wakati leseni ya kucheza inatolewa na TFF. Vilevile tumeziagiza klabu kulipia ada za ushiriki kwa kila timu; leseni za wachezaji, ada za wachezaji na ada za mikataba. Mchezaji hatapewa leseni ya kucheza kama uongozi wa timu hautakamilisha taratibu za malipo.

TFF linapenda kuzikumbusha timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwamba hatutatoa leseni ya mchezaji yeyote ambaye timu haikuleta mkataba wakati wa maombi ya usajili, hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 68 vipengele vya 1, 2, 3 na 8 ya Ligi Kuu ya Tanzania toleo la 2016/2017.

Kila timu inatakiwa kuleta nakala tatu za mkataba wa mchezaji, ili kamati ya katiba, sheria na hadhi za wachezaji iweze kupitia na TFF iweze kuidhinisha mikataba hiyo. Baada ya hapo timu na mchezaji, watakuja kuchukulia mikataba hiyo hapa TFF. 

No comments:

Post a Comment