Simba
ilikuwa ikimtuhumu Kessy kuvunja mkataba kwa kuanza kuvaa jezi, kufanya
mazoezi, kusafiri na kushiriki shughuli mbalimbali za mabingwa hao wa VPL msimu
uliopita wakati muda wa mkataba wake na Wekundu hao wa Msimbazi haujafika
kikomo.
Kamati
hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Richard Sinamtwa imepitia usajili wa timu zote
na kujiridhisha kwamba suala la mchezaji Hassan Kessy limeegemea kwenye madai
na si usajili ambako Simba ndiye mdai kwa kumtuhumu mchezaji huyo kuwa alianza
kuitumikia Young Africans kabla ya kumaliza mkataba wake Simba SC. Mkataba wake
ulifika mwisho, Juni 15, 2016.
Kama
ni madai Simba inaweza kuendelea kumdai Kessy au Young Africans wakati mchezaji
huyo anatumika uwanjani kwa mwajiri mpya. TFF inafuatilia na kuangalia haki ya
Simba namna ya kupata haki yake baada ya kuwasilisha madai kuhusu kuvunja
mkataba na mwajiri wake wa zamani.
Kanuni
hazimzuii mchezaji kuendelea kucheza kwa hoja ya madai badala yake suala hilo
linaweza kumalizwa wakati mashindano yanaendelea. Kamati inaendelea kupitia
malalamiko na pingamizi za wachezaji wengine na inatarajiwa kutoa taarifa rasmi
kuhusu wachezaji wote wakati wowote kuanzia sasa.
No comments:
Post a Comment