Home Traders

Home Traders

Tembelea TK FM Redio 88.5 Tanga

Wednesday, 3 August 2016

Mghana atta aanza majigambo azam fc

WINGA mpya wa Azam FC, Enock Atta Agyei aliyesajiliwa kutoka Medeama SC ya Ghana  ameanza majigambo katika timu yake  mpya ya azam na kusema kuwa amekuja kukata kiu ya mabao katika timu hiyo.
Kinda jipya la Azam Enock Atta Agney

Aidha Atta amesea kuwa  amefurahi sana  kuwa Azam fc  na amekuja kushinda makombe pamoja na kuweka historia  ndani ya timu hiyo kabla  hata hajaondoka huku akisema kuwa amejiandaa kuzikabili changamoto  zote zilizopo mbele yake .

Tayari nyota huyo ameshasaini mkataba wa miaka miwili kuwatumikia mabingwa hao akipewa jezi namba 10, ambapo jana aliweza kuanza rasmi mazoezi na wachezaji wenzake huku akionekana kuwafurahisha zaidi makocha kwenye mazoezi hayo

Hata hivyo kuhusiana na utofauti kati ya Tanzania na Ghana amesema kuwa  moja ya utofauti mkubwa wa soka la Tanzania na Ghana ni namna ya uchezaji, Ghana wakicheza soka la kumiliki mpira na nguvu tofauti na Tanzania huku akidai kuwa aina yao ya uchezaji ndio iliyofanya wakapata matokeo bora dhidi ya Yanga.

“Ni vizuri kwangu kuwa hapa, bado sijalijua sana soka la hapa, najua soka la Ghana lipo juu kuliko hapa, lakini unapokuwa mchezaji unahitaji kubadilisha mazingira, unatakiwa kuhama timu bila kujali nini kitatokea na cha muhimu ni kupambana wewe mwenyewe kwa kufanya kazi kwa bidii,” alisema.

Mipango yake ya baadae kwa mchezajji huyo  kucheza Ulaya, lakini amedai kuwa  si lazima sana  kucheza huko ili afanikiwe bali hata Afrika panatosha na  kumfanya mtu kuwa  na maisha bora cha msingi ni yeye kufanya kazi kwa bidii.

“Kila mchezaji anaheshimu kucheza soka Ulaya, hii ni kutokana unapocheza Ulaya unaweza kutatua matatizo yako mengi kwenye maisha, hayo ni kwa mujibu wa maneno ya watu, lakini mimi naamini ya kuwa popote panaweza kuwa Ulaya inategemeana na wewe unaifanyaje kazi yako.

No comments:

Post a Comment