Home Traders

Home Traders

Tembelea TK FM Redio 88.5 Tanga

Tuesday, 2 August 2016

Mo akunjuka na Milioni 100 za Usajili Simba

MFANYABIASHARA Mohamed Gulam Dewji ametoa mfano wa hundi Sh. Milioni 100 kama mchango wake katika usajili wa klabu hiyo kuelekea msimu ujao.
Mo Dewji ametoa mfano wa hundi hiyo leo ofisini kwake, Jijini Dar es Salaam akimkabidhi Rais wa Simba SC, Evans Aveva.

Kufuatia mchango huo wa Dewj AVEVA amemshukuru Dewj kwa msaada huo huku akisema kuwa bado timu inahitaji  Sh. Milioni 320 kukamilisha usajili, ingawa hakusema bajeti nzima ya usajili ya klabu hiyo ni kiasi gani.

“Ninashukuru sana kwa msadaa huu kutoka kwa mwanachama wetu, na sasa ninashukuru tunaweza kumsajili Frederick Blagnon kutoka Ivory Coast,”alisema Aveva.
Na wakati akipokea mfano wa hundi hiyo leo, Aveva alisema ameyakubali mabadiliko kwa moyo mmoja na atayasimamia kuhakikisha yanakwenda haraka ili kutimiza azma ya Simba kuwa ya kutisha siyo tu Tanzania, bali Afrika nzima.
Pamoja na hayo, Aveva akawataka wanachama zaidi wa Simba kuchangia sehemu iliyobaki, Sh. Milioni 320 katika bajeti ya usajili ya klabu.

No comments:

Post a Comment