Msomaji wa Tanga Kunai leo kwa faida ya wanatanga basi ni bora tukakumbushana na kuifahamu historia vizuri,huku tukijikita kabisa kujua kumbe shule ya kwanza Tanzania hii ilijengwa Tanga?sasa kwanini ilijengwa Tanga tuendeleeee na mtiririko huu hapa chini!!!
MWAKA 1848, Mmishenari wa Kijerumani Dk Johan Ludwig Krapf, alitembelea kijiji cha Magila kilichopo Muheza mkoani Tanga akiwa katika safari zake za Afrika Mashariki.
MWAKA 1848, Mmishenari wa Kijerumani Dk Johan Ludwig Krapf, alitembelea kijiji cha Magila kilichopo Muheza mkoani Tanga akiwa katika safari zake za Afrika Mashariki.
Magila kuna mlima ulio katika safu za milima ya
Usambara ukipakana na mlima wa Magoroto ambao ndio chanzo cha maji ya
mto Mkurumuzi unaoelekea Muheza.
Historia inaonyesha eneo la mlima Magila wenye
miamba na mawe mengi, zamani kabla ya kuja wageni lilitumika kuwatenga
wagonjwa wa ukoma na magonjwa mengine yasiyotibika, kwa lengo la
kuwazuia wasiwaambukize wengine.
Dk Krapf alipofika na kuwaona wagonjwa hao
waliokuwa wakiishi kwa madhila makubwa, alichonga msalaba katika mti wa
mkuyu kwa imani kuwa Mwenyezi Mungu angewaponya wagonjwa hao.
Eneo hilo ndilo lililokuja kujengwa shule ya
kwanza na Waingereza mwaka 1886. Alama ya msalaba huo ipo hadi na sasa
na ndipo ilipo Shule ya Sekondari Hegongo.
Hadi leo mahali hapo panaitwa Magila Msalabani.
Kwa sasa Magila ni kata yenye vijiji vya vya Magila, Mikwamba, Misongeni
na Mafleta.
Nilifika katika eneo hilo nilipokuwa wilayani Muheza hivi karibuni ili kuchunguza historia ya eneo hilo.
Hapo nikutana na Luteni Kanali mstaafu John Mhina
ambaye amekamilisha kuandika kitabu kuhusu historia ya Magila Msalabani,
kinachoeleza historia ya kijiji hicho na ujio wa wazungu walioanzisha
shule ya kwanza Tanganyika na kanisa.
Luteni Kanali Mhina aliyelitumikia Taifa kwa muda
mrefu kama mwanajeshi , na baadaye kuwa Mbunge wa Muheza kutoka mwaka
1990 hadi 1995, anasema harakati za kuanzisha shule katika kijiji hicho
zilitokana na Wamishenari waliokuja Afrika Mashariki kutoka Ulaya
kwaajili ya kueneza dini ya kikristo tangu miaka ya 1770.
Anawataja baadhi ya Wamishenari hao kuwa ni pamoja na David Livingstone, Charles Mackenzie, William Tozer na Edward Steer.
Anasema harakati hizo zilianzia tangu visiwa vya
Zanzibar mwaka 1863 ambako pia walikomesha biashara ya utumwa na kuanza
ujenzi wa kanisa la Anglikana la Mkunazini Zanzibar kwa miaka 10 tangu
mwaka 1873.
Anasema wakati huo kulikuwa na shule iliyoanzishwa
Zanzibar maeneo ya Kiungani na Kiinua mguu na Askofu William Tozer
mwaka 1869. Hata hivyo, anasema shule hiyo haikuwa rasmi na ilikuwa
ikifundisha elimu ya dini kwa watumwa waliokombolewa.
Uamuzi wa kujenga shule Bara
“Mnamo Agosti 13, 1967 Askofu Tozer alimtuma Padri
CA Alington aende Vuga (Lushoto) kwa Chifu Kimweri ili apate kibali cha
kujenga kituo cha misheni kwenye maeneo ya Bara,’’anasimulia Luteni
Kanali Mhina na kuongeza:
“ Padri Alington alimchukua Vincent Mkono
aliyekuwa mwanafunzi wake wa Kiungani na mwingine Mwinyi Khatib
aliyekuwa mkalimali. Msafara huo ulipata baraka za Sultan Majid
aliyekuwa akitawala Zanzibar.”
Anaeleza kuwa baada ya msafara wao kufika Vuga, Chifu Kimweri aliwasikiliza, lakini akaomba apewe muda wa kutafakari kwanza.
Baadaye Januari 20, 1868, Padri Alington
alirudi Vuga na kuruhusiwa na Chifu Kimweri kujenga sehemu yoyote katika
maeneo ya Pwani.
Anasema Padri Alington aliamua kuchagua eneo la
Magila ambalo lilikwishajulikana kutokana na alama ya msalaba uliowekwa
na Dk Krapf.
“ Jumbe Kifungiwe aliyekuwa akiongoza Magila
wakati huo chini ya baraza la ‘wamaka’ (Baraza la Wazee wa Kibondei),
walimpa mlima wote wa Magila wakidhani kuwa atashindwa kujenga kwa
sababu ya kuwa na mawe mengi….kwa mshangao aliporudi aliyatumia mawe
hayo kujengea.” anaeleza.
Anasema pamoja na kazi ya kueneza dini Wamishenari hao walijipa jukumu la kuwatunza wagonjwa wa ukoma na kuanzisha shule.
“Shule ya sokoni ilikuwa kwanza kujengwa maeneo
hayo mwezi Aprili 1869 chini ya Padri Fraser na wanafunzi wake walikuwa
ni pamoja na Jumbe Kifungiwe na ndugu yake Sagosago na vijana wengine.
Palikuwa na soko dogo na mti mkubwa wa Mzindanguuwe, watu wazima
walipenda kukaa hapo ili walione jambo hilo geni,” anaongeza kusema.
Sekondari ya Hegongo
Hivi sasa eneo hilo kuna shule iitwayo Hegongo. Mkuu wa shule hiyo, Wilfred
Mdimu anasisitiza kuwa eneo hilo ndipo palipojengwa shule ya kwanza
Tanzania ambapo mpaka sasa kuna mabaki ya darasa la kwanza
lililojengwa na Wamisheni.
Hivi sasa anasema darasa hilo linatumiwa kama ofisi ya walimu wa shule ya sekondari ya kata Magila.
“Hili ndilo darasa la kwanza lililojengwa mwaka 1869 na
Waingereza. Awali lilikuwa ghorofa lakini likabadilishwa. Inasemekana
shule nyingine ilijengwa Bagamoyo na baadaye Minaki,” anasema Mdimu na
kuongeza,
“Walijenga pia kanisa baada ya lile la Mkunazini
Zanzibar. Lakini lilipochakaa ndipo wakajenga kanisa jingine mwaka 1886
kama lile la Mkunazini na ndiyo linatumika hadi sasa.”
Akizungumzia uchaguzi wa eneo hilo, Mdimu anasema
awali wazungu walitaka kujenga shule maeneo ya Muhenza Mkumbi na
Mkanyageni, lakini wakaathiriwa na malaria, ndipo wakahamia katika
mlima wa Magila.
Kuhusu shule hiyo, Mdimu anasema kuwa awali
ililenga kuwaandaa Waafrika ili wawasaidie wamisheni katika kazi zao.
Waliwafundisha kusoma, kuandika na kuhesabu.
Baadaye elimu ikapanuka baada ya shule za St. Marys na St Martin kujengwa zikiongeza masomo na wanafunzi.
Anaongeza kuwa shule hizo hazikudumu muda mrefu,
bali zilibadilishwa na kuwa Sekondari ya wasichana ambayo nayo ilikuja
kuhamishiwa wilayani Korogwe ilipo shule ya wasichana maarufu kwa jina
la Korogwe girls.
Baada ya kuhamisha shule hiyo, matumizi
yakabadilishwa na kikaanzisha chuo cha ualimu kwa wanawake tu. Hata
hivyo, anasema chuo hicho nacho kilihamishiwa tena Korogwe kilipo chuo
cha ualimu hadi leo.
“ Mwaka 1974 hadi 75, majengo hayo yakafanywa kuwa
mahali pa kujifungulia wanawake na ndipo ilipoanzia hospitali teule ya
Muheza. Lakini ikahamishiwa eneo ilipo sasa na majengo haya yakabaki
matupu,” anasema Mdimu.
Kuanzishwa kwa Hegongo sekondari
Mwalimu Mdimu anasema baada ya majengo kubaki
matupu, mwaka 1976 wenyeji wa Magila walimwomba Askofu wa kanisa hilo
dayosisi ya kaskazini John Ramadhani, ili waanzishe shule ya sekondari
hasa kwenye majengo ulipo msalaba wa Dk Krapf, naye akawakubalia.
“Februari 24, 1977 shule ya Hegongo ilianzishwa
ikiwa chini ya wenyeji wa Magila ili kuwapa elimu watoto wa wilaya
hiyo,” anasema.
Hata hivyo anasema shule hiyo haikuwa na maendeleo
mazuri kwa muda mrefu. Isitoshe, wasimamizi wa shule hiyo walishindwa
kuiendesha kutokana na madeni makubwa ya umeme, mishahara ya watumishi
na mafao yao.
Hegongo ya sasa
Anasema hadi mwaka 2000 wasimamizi wa shule hii walishindwa kabisa kuiendesha wakairudisha kwa kanisa.
“Tangu wakati huo uongozi wa kanisa umeamua
kuiendesha kwa kwa kulipa madeni makubwa yaliyokuwepo na kuimarisha hali
ya elimu,” anasema na kuongeza:
“Kwa sasa tunaboresha majengo, tumejenga maabara,
maktaba ya kisasa na tutaongeza nyingine. Askofu wa sasa ameamua
kuwachukua mapadri 10 waliomaliza kidato cha sita na kuwapeleka vyuo
vikuu ili wasomee ualimu kwa ajili ya shule hii.’’
Kwa upande mwingine, majengo ya zilizokuwa shule
za St. Mary’s na St. Martin sasa zimechukuliwa na Serikali, huku
mojawapo ikitumika kama shule ya sekondari ya kata ya Magila na nyingine
kama shule ya msingi.
Safi
ReplyDelete