Mamia ya wahamiaji wamekufa maji wakati
wakijaribu kuelekea nchini Italia kupitia Bahari ya Meditarian ambapo
boti yao ilizama karibu na kisiwa cha Malta wakati wakijaribu kuelekea
nchini Italia.
Manusura wawili raia wa Palestinian wamelieleza
shirika la kimataifa la uhamiaji la IOM jinsi ajali hiyo ilivyotokea na
kwamba ilisababishwa na vurugu kati ya abiria hao na wafanya biashara za
magendo..
Msemaji wa shirika la IOM Leonard Doyle ameiambia BBC
kuwa watu wawili walionusurika katika ajali hiyo wamesema mazingira ya
kuzama kwa boti yao ilitokea pale walipolazimishwa kuhamia katika chombo
kingine na walipokataa vurugu ikaanza.
Doyle anasema kuwa watu hao wamesema kuwa walianza safari hiyo katika bandari ya Damietta nchini Misri Septemba wakiwa 500.
Shirika
la umoja wa mataifa linasema wahamiaji wapatao 130,000 wamefanikiwa
kuingia Ulaya kupitia bahari ya Mediteranian ambapo kwa mwaka huu pekee
wahamiaji 80,000 wamepitia njia hiyo.
Kwa mjibu wa ripoti ya umoja wa mataifa Italia imepokea wahamiaji 118,000.
Chanzo BBC
No comments:
Post a Comment